Na Mwandishi Maalum, Madrid Spain.
Vivutio vya Utalii vinavyopatikana nchini vimeonesha kuvutia washiriki wengi katika Maonesho ya Utalii ya FITUR yanayoendelea nchini Hispania.
Kaimu Meneja wa Mikutano na Matukio wa Bodi ya Utalii (TTB) inayoratibu maonesho hayo kwa upande wa Tanzania Bi. Lily Fungamtama amesema kuwa wamepokea mawakala wengi wa utalii walioonesha kuvutiwa na vivutio hivyo na kuweka miadi ya kuvitembelea katika siku za usoni.
Hispania ni miongoni mwa masoko makubwa yanayoleta watalii nchini ikiwa inashika nafasi ya 11 kwa kuleta watalii nchini.
Maonesho hayo ya siku tano yanatarajiwa kuchukua siku tano na kumalizika Jumapili ijayo.
0 Comments