Header Ads Widget

CCM SONGWE YAPITISHA WOTE KATA 94 WALIONGOZA KURA ZA MAONI, VIGOGO WALIOTEGEMEA “HURUMA” WAKWAMA

 

Na Moses Ng’wat, Songwe.

Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe imepitisha wagombea wote walioongoza kura za maoni katika kata zote 94, huku vigogo wawili waliokuwa wakisubiri “huruma” ya chombo hicho cha mwisho cha uteuzi wakikosa kupata nafasi.

Vigogo hao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma na diwani wa Kata ya Mwaka Kati mjini Tunduma, Ayoub Mlimba, pamoja na mwenzake wa Halmashauri ya Momba na diwani wa Kata ya Mkulwe, Mathiew Chikoti ambao rasmi wametupwa nje kufuatia kushika nafasi ya pili kwenye mchakato wa kura za maoni, huku wakiteggemea 'huruma' za kikao hicho majina yao kurejeshwa.

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Songwe, Yusuph Rajabu, alisema jana kuwa kikao cha Halmashauri Kuu kilichofanyika Agosti 13, 2025, kimepitisha majina yote kwa mujibu wa Ibara ya 89 ya Katiba ya chama hicho.

“Mkoa wetu una wilaya nne, majimbo sita ya uchaguzi, tarafa 12 na kata 94. Kwenye kata zote hizi, wagombea waliopata kura nyingi kwenye kura za maoni wote wamepitishwa na hakuna hata jina moja lililoenguliwa, hivyo hivyo na kwa viti maalumu hakuna jina lililoenguliwa,” alisema Rajabu.

Alibainisha kuwa kikao hicho cha ngazi ya mwisho cha uteuzi kwa nafasi za wagombea wa udiwani kimetekeleza jukumu hilo 

mujibu wa Ibara ya 89 ya Katiba ya chama hicho, huku akiongeza kuwa hatua inayofuata ni maandalizi ya wagombea kuchukua fomu za uteuzi kuanzia Agosti 14 hadi 27, 2025, kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mwenezi Rajabu alisisitiza kuwa CCM Songwe itahakikisha wagombea wote wanachukua fomu kwa wakati, kwa kushirikiana na makatibu wa wilaya, huku chama kikiendelea kuimarisha mshikamano wake kuelekea uchaguzi.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI