Header Ads Widget

TAKWIMU ZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NCHINI ZAONGEZEKA KWA KASI







 

KWAMUJIBU wa Takwimu za kamisheni ya umasikini na magonjwa yasio ambukiza Tanzania zinaonyesha kuwa kuna ongezeko kubwa la magonjwa yasiombukizwa nchini kwa rika mbalimbali hadi kufikia asilimia 41 ya vifo na majerihu........Na Hamida Ramadhan Dodoma 



Kutokana na na hayo Wizara ya Afya imeombwa kutojikita  katika mikakati ya kupambana juu ya tiba ya magonjwa hayo na badala yake Wizara izingatia kinga zaidi.


Kauli hiyo imetolewa na Dkt Emmanuel Makundi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR katika Hafla iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) jijini hapa. 


Amesema, ongezeko la magonjwa yasiyo ambukiza limekuwa na changamoto kubwa nchini Tanzania  hasa katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ambapo tofauti na mtazamo uliopo kuwa wazee ndio wanaougua hayo.


"Takwimu zinaonyesha kwamba kuna ongezeko kubwa la magonjwa yasiombukiza kwa vijana hususani shinikizo la damu na Kiharusi kutokana na hayo niwazi kuwa sekta ya afya pekee haitoweza kupambana na tatizo hili hivyo kuna haja ya kuchukua hatua madhubuti na zinazohusisha sekta mbalimbali  ili kupambana na tatizo hili,"amesema 



Awali akifungua hafla hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi,Teknlojia na Ubunifu (COASTECH) mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa COASTECH Dkt, Wilbert Manyilizu amesema,lengo la warsha hiyo ni kuwashirikisha Wadau wakuu wa matokeo ya tafiti za kisayansi na Teknolojia ili waweze kuwasilisha na kutoa matokeo ya tafiti zao.                                 

Amesema,COSTECH iliwaita watafiti katika Sekta nne za awali ambazo ni sekta ya Afya,Kilimo,maliasili na mifugo  ili wawasilishe tafiti zao ambazo hufanyiwa kazi na Tume hiyo ambayo ndio yenye dhamana ya kuishauri Serikali katika masuala ya sayansi na teknolojia.


Aidha amesema,lengo la kuanzishwa kwa Tume hiyo ni  kuishauri Serikali katika masuala ya sayanasi na Teknolojia na ubunifu huku akisema,jukumu kubwa la COASTECH ni kuratibu na kuhamasisha Mambo ya utafiti na ubunifu ambapo katika jukumu hilo pia kuna majukumu mengine.


Ameyataja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kusimamia Menejimenti ya maarifa yanayopatikana katika ubunifu na utafiti na baadae kusambaza kwa Wadau huku akisema, michakato yote ya kuwatambua na kuwawezeaha wabunifu ni jukumu lao.


Aidha amesema,jukumu lingine la Tume hiyo ni kuhabarisha Wanachi na Wadau mbalimbali kwa kukusanya na kusambaza taarifa za sayansi  na ubunifu wa wananchi pamoja na kusambaza vijarida.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI