Header Ads Widget

TAKUKURU WABAINI MAPUNGUFU MIRADI 19 MKOANI LINDI

 




NA HADIJA OMARY_LINDI...


Ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi, thamani ya fedha kwa baadhi ya miradi, ukiukwaji wa taratibu za manunuzi  na ushirikishwaji mdogo wa wadau katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo ni miongoni mwa mapungufu yaliyobainika katika ukaguzi wa Miradi 19 iliyokaguliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Lindi



Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/2022 oktoba 2021 hadi Desemba  2021 Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi Mhandisi Abnery Mganga kwa Waandishi wa Habari alisema kuwa katika kipindi hiko kupitia dawati la uzuiaji Rushwa ilifuatulia matumizi ya fedha ya zaidi ya bilioni 12 katika miradi 19



Alisema ukaguzi huo ulihusu seka ta kilimo miradi 8, Sekta ya Afya 2, sekta ya ujenzi mradi 1 huku sekta ya elimu ikiwa na miradi 8



Hata hivyo alieleza kwamba mapungufu hayo ambayo yangeweza kusababisha mianya ya Rushwa yameweza kufanyiwa kazi kwa kufanya vikao na wadau wa miradi husika pamoja na kutoa Elimu kwa lengo la kuondoa mianya ya Rushwa  iliyopo  pamoja na kuimarisha usimamizi wa miradi kwa kusisitiza uzingatiaji wa sheria na kanuni za Manunuzi ya Umma ili kupata miradi bora yenye kukidhi thamani ya fedha.




Pamoja na mambo mengine Mhandisi Mganga alieleza kuwa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022 January hadi machi  2022 Taasisi hiyo imejipanga  kuendelea na ufuatiliaji wa fedha za  miradi ya Maji na ujenzi wa Barabara  chini ya TARURA katika halmashauri zote ndani ya Mkoa huo wa Lindi. 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI