Header Ads Widget

KWA KAZI KUBWA ZA RAIS DKT SAMIA, AHSANTE YETU OKTOBA NI KUTIKI TU– GRACE TENDEGA

Na Matukio Daima, Iringa

Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kwa nyakati mbili tofauti kupitia vyama vya Jahazi Asilia na CHADEMA, Grace Tendega, ameibuka upya kwa kutoa pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa “ahadi na shukrani ya Watanzania kwa Rais huyu shupavu ni kuhakikisha Oktoba mwaka huu kila mmoja anatiki  CCM kwa Dkt Samia na  CCM.

Grace Tendega ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Viti Maalum anayemaliza muda wake kupitia CHADEMA, alisema hayo alipokuwa akizungumza na Matukio Daima Media,   Tendega ambae ni mkazi wa Kijiji cha Tagamenda kata ya Luhota jimbo la Kalenga  mkoani Iringa alisema kazi za Rais Dkt Samia ni kubwa sana.

 Alisema anatambua  mchango mkubwa wa Rais Dkt Samia katika kuleta maendeleo ya kweli na shirikishi,  kuwa utawala wa awamu ya sita umeleta heshima kwa Tanzania kitaifa na kimataifa.

“Tanzania kuvunjia rekodi kwa kuongozwa na Rais mwanamke ni tukio la kihistoria, lakini kilicholeta heshima kubwa zaidi ni namna alivyoiongoza nchi kwa weledi, busara na kasi ya maendeleo inayogusa kila mtanzania,” alisema Tendega.

Alisema Rais Dkt  Samia amevuka matarajio ya wengi waliokuwa na mashaka kuhusu uwezo wa mwanamke kushika nafasi ya juu ya uongozi, akieleza kuwa dunia nzima sasa inashuhudia na kupongeza utendaji wake.

Kwa mujibu wa Tendega, mafanikio ya Rais Samia si tu yameinua heshima ya Taifa, bali yamewaheshimisha wanawake wote duniani kwa kuonesha kuwa jinsia si kigezo cha udhaifu katika uongozi, bali uwezo, maono na uzalendo ndivyo vinavyotakiwa.

“Kwa miaka mingi Tanzania haijawahi kupata Rais mwanamke tangu uhuru, na wengi walikuwa na mashaka lakini leo hii, kila mmoja anajivunia kuwa na Rais Dkt Samia kutokana na kazi kubwa aliyofanya. Tumeshuhudia mabadiliko ya kweli,” alisema Tendega.

Akitolea mfano wa miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya utawala wa Rais Samia, Grace alisema maendeleo yameonekana kuanzia ngazi ya Taifa hadi vijijini, na kwamba miradi hiyo inawanufaisha wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.

“Kuna mabadiliko makubwa mkoani Iringa. Miradi ya maji, barabara, elimu na afya inaendelea kutekelezwa kwa kasi kubwa Kwa kweli, wananchi ni mashahidi wa haya yote,” alisisitiza.

Ameeleza kuwa katika suala la maji pekee, Rais Dkt Samia ameandika historia kwa kuleta mapinduzi makubwa ya huduma hiyo ya msingi, jambo lililowarahisishia maisha wanawake wa vijijini waliokuwa wakiteseka kwa umbali wa kutafuta maji.

“Maji hayamhusu mwanamke peke yake, lakini ukweli ni kwamba mwanamke ndiye aliyekuwa akiteseka zaidi leo hii, wanawake wanatulia nyumbani, wanajihusisha na shughuli za uzalishaji badala ya kutumia masaa mengi kutafuta maji,” aliongeza.

Aidha, Tendega ametaja hatua ya serikali ya kuwarejesha shuleni watoto wa kike waliopata ujauzito kama moja ya mafanikio makubwa ya utawala huu, akieleza kuwa hilo ni tendo la kiubinadamu na la kihistoria katika kupigania usawa wa kijinsia na haki za mtoto wa kike.

“Hii ni serikali ya watu Wanafunzi sasa wanasoma bila ada, watoto wa kike waliokatishwa masomo kwa sababu ya ujauzito wamerudishwa shuleni. Hizi ni hatua kubwa ambazo zinapaswa kuungwa mkono,” alisema.


Amesisitiza kuwa kazi kubwa ya Rais Samia si tu imekijengea heshima Chama cha Mapinduzi (CCM), bali pia imekiimarisha kwa vitendo kwa wananchi waliokuwa na mashaka na siasa.

“Rais Samia amekiheshimisha chama chake na amekiheshimisha taifa tumeshuhudia siasa zenye maridhiano, utulivu wa kitaifa, na maendeleo yasiyoangalia tofauti za kisiasa hili ni jambo la kujivunia,” alieleza.

Tendega alitoa wito kwa wananchi wote kuhakikisha kuwa Oktoba 2025 wanajibu kwa vitendo kazi kubwa ya Rais kwa kutiki CCM, ili aendelee kutimiza dhamira yake njema kwa Watanzania.

“Ahadi yetu kwa Rais Dkt Samia ni kura zetu tunapaswa kumrudishia heshima kwa kumuwezesha aendelee na kazi aliyoianza. Tanzania bado inamhitaji,” alisisitiza.

Kauli ya Grace Tendega imekuwa ikiungwa mkono na wana CCM  ndani ya jimbo la Kalenga na nje ya Kalenga ambapo tayari baadhi ya wadau wa maendeleo na wananchi wamekuwa wakimtaja kama mmoja wa watu muhimu wanaoweza kutia nia ubunge jimbo la Kalemga na akawavusha .

kuwa  kutokana na misimamo yake bungeni  na jinsi amekuwa akijenga hoja na kuwasemea wananchi wengi wanaamini akigombea jimbo na kuwa mbunge atawafaa zaidi.

Kwa sasa, uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 unazidi kusogea huku viongozi mbalimbali wakiendelea kujitokeza kuunga mkono juhudi za serikali na kueleza dhamira zao kwa ajili ya taifa.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI