Na Hamida Ramadhan Dodoma
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ametoa siku saba kwa vyombo vya dola kuhakikisha wanapeleka taarifa ya uchunguzi Ofisi ya Rais kuhusu Mauwaji ya Watu wa tano wa Familia Moja yaliyotokea katika Kata ya Zanka ,kijiji cha Zanka Wilaya Bahi Mkoani Dodoma.
Ameyesema hayo leo Januari 26 2022 alipotembelea na kuwapa mkono wa pole wafiwa kijijini hapo Mkoani Dodoma ambapo amesema matukio hayo ni unyama wa Hali ya juu hayawezi kukubalikia huku akilitaka jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuweka kambi na kuhakikisha ndani ya Siku saba wauaji wawewamepatikana na kufikisha katika vyombo vya dola ili nawao wapate haki yao.
“Serikali imesikitishwa na tukio hili la hovyo hivyo na matukio kama haya yamekuwa yakikitokeza kwa wingi katika nchi yetu sasa nivitake vyombo vya ulinzi na usalama kuwa macho na taarifa hizi zifikushwe kwa IGP Saimon Siro na kuhakikisha matukio kama haya yanakaoma mara moja katika nchi yetu,”Amesema Makamu Dkt Mpango.
Hata hivyo ameitaka jamii kupendana na kuwa ha tabia ya kujuliana hali huku akieleza "Nimesekitiswa na wananchi wa hiki kijiji hivi inawezekanaje watu wanauawa nadani siku tatu mpaka wanaharibika eti jirani,rafiki na ndungu wala Uongozi wa kijiji hawana taarifa hapana hapa kunatatizo kubwa," amesema Makamu wa Rais Dkt Mpango.
Mauaji hayo yalijulikana tarehe 22 saa 10 jioni huku miili ya watu hao ikikutwa ndani ikiwa imeshaanza kuharibika ambapo marehemu hao walitambuliwa kwa majina ya Hoseah Kipande baba wa familia mke Paulina Kipande na watoto wawili Isack Kipande mwanafunzi wa kidato cha Kwanza ,Agines kipande mwanafunzi wa darasa la tatu na Mjukuu aliyejulikana kwa jina la Heltony ambaye ni mwanafunzi wa darasa la Nne.
Mwisho.
0 Comments