Na Andrew Chale, Dar es Salaam.
SERIKALI ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa, watakuwa wanaweka mezani takwimu za ugonjwa wa UVIKO _19 ilikuwawezesha Watanzania kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya zao ikiwemo kuchanja na kujikinga.
Waziri Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo leo Januari 26,2022 wakati wa kupokea dozi ya awamu ya pili kutoka Serikali ya China ambao wametoa chanjo dozi 800,000 aina ya Sinopharm, tukio lililofanyika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKN terminal 2, Dar es Salaam.
Katika hatua hiyo, amemwagiza Mganga Mkuu wa Serikali kuwa anatoa taarifa za UVIKO 19 kila wiki ili wananchi wachukue hafua sahihi.
Waziri Ummy Mwalimu amemshukuru Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Balozi Chen Mingjian kwa msaada huo huku akimwakikishia kuendeleza ushirikiano wa nchi hizo mbili.
"Hii ni awamu ya pili kutoka kwa rafiki zetu Serikali ya China.
Awamu ya kwanza tulipokea dozi 500,000aki ambazo zingeweza kuchanja watu 250,000.
Kwa taarifa kutoka kwa Meneja wa Mpango wa taifa wa Chanjo, Chanjo zote wamenihakikishia zimekwisha." Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Ambapo amewashukuru wadau wote wa kimaendeleo wa ndani na nje katika masuala ya kupambana na virusi vya UVIKO 19.
"Hizi dozi tulizopokea leo zitatuwezesha kuchanja wananchi Laki nne.
Kwa niaba ya Rais wetu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Tunasema asante sana na mzigo huu utakaa muda mchache." Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha, Waziri Ummy Mwalimu ametoa takwimu za jumla ya chanjo zote zilizopokelewa Tanzania hadi sasa.
"Tanzania tumepokea jumla ya chanjo dozi zaidi ya Milioni 8.8. Chanjo hizo zikijumlisha za Sinopharm, Janssen, Moderna na Pfizer ambazo zinatosha kuchanja Wananchi zaidi ya Milioni tano.
Hiyo ndo idadi ya chanjo ambazo tunazo." Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Akitoa takwimu za UVIKO 19 Duniani kote, ambapo alibainisha kuwa, kwa ujumla mwenendo huu hadi Jumapili usiku Januari 23,2022, Duniani kote wamethibigika watu zaidi ya milioni 349. Huku watu zaidi ya milioni 5 wakipoteza maisha.
Aidha kwa Tanzania, Waziri Ummy Mwalimu alibainisha;
"Hadi Januari 23,2022 waliothibitika kuwa na maambukizi ya UVIKO 19, takwimu ambazo tunazo jumla ya watu Elfu 33,000 wanamaambukizi, na watu 781 waliopoteza maisha, kwa hiyo tunatoa pole kwa walipoteza wenza wao na tutaendelea kutoa elimu na hamasa ya ugonjwa huu." Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha, alitaja takwimu za waliochanja hadi sasa ni kuwa mpaka kufikia Januari 25,2022 ni jumla ya watu milioni 1.9 ambayo ni sawa ya asilimia 3.3 ya Watanzania ambao walikuwa wamelengwa kuchanjwa." Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha, amemwagiza Mganga mkuu awe anatoa takwimu kila wiki kwa waliochanja.
"Habari njema hadi sasa hakuna mtu aliyepata madhara kutokana na chanjo.
Kama kuna mtu amepata madhara aje anione mimi mwenyewe Waziri...Tutaendelea kuangalia mwenendo kwa mikoa yote." Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Na kuongeza:
"Tumeangalia idadi kubwa ya wanaokuwa wanalazwa na wanaokuwa na ugonjwa mkali ama kufariki, kwenye Hospitali zetu na vituo vya kutolea huduma za afya zaidi ya asilimia 90 ni ambao hawajachanjwa chanjo ya UVIKO 19.
Aidh, takwimu hizi tumeziangalia kuanzia mwezi September, hivyo wakachakua kuanzia September 2021hadi January 23,2022, kati ya wagonjwa waliolazwa 3,147 kati yao wagonjwa 2,990 walikuwa hawajachanja, kwa hiyo asilimia 95." Alisema.
...wagonjwa mahututi 31 walioripotiwa kwa siku ya Januari 23, 30 sawa na asilimia 97 walikuwa hawajapatq chanjo.
Lakini katika kipindi hiki bifi 76 viliripotiwa ambapo vifo 73 sawa na asilimia 97 vilikuwa ambao hawajachanjwa. alisema Waziri.
Waziri Ummy aliwaomba wananchi kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO 19 kwa kukamilisha idadi kamili ya dozi na kwa wakati kama inavyoshauiwa na wataalam ili kukinga ugonjwa huo wa UVIKO 19.
Kwa upande wake Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Balozi Chen Mingjian alisema Watanzania na China wana undugu na ushirikiano wa muda mrefu hivyo watazidisha mashirikiano hayo.
0 Comments