Teddy Kilanga _Arusha
Waziri wa kilimo Hussein Bashe ameitaka Mamlaka ya afya ya mimea kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha maabara zote za mimea zisajiliwe ili zitambulike na Serikali ya Tanzania kuwa zinatoa huduma kwa wakulima.
Sambamba na hilo serikali imesema itaanzisha vituo maalumu katika maeneo ya nyanda za juu kusini,kanda ya kaskazini na Dar es Salaam kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao sambamba na halmashauri kutoa leseni maalum bila malipo hasa kwenye wanunuzi wa mazao ya parachichi.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka wa 15 wa biashara ya horticulture,Waziri kilimo Hussein Bashe amesema vituo hivyo vitatoa huduma zote ambayo itakuwa rahisi katika kuwahudumia wazalishaji na wanunuzi wa maeneo yote ili mazao hayo yanaposafirishwa nje ya nchi yaonekane yamezalishwa nchini Tanzania.
"Sio dhambi mkenya kununua parachichi nchini Tanzania tatizo ni asili ya mahali lilipozalishwa zao hilo na ili kuondoa changamoto hiyo ni kuanzisha vituo ambavyo vya kuongeza thamani ambavyo vitashughulikia masuala yote ikiwemo uhifadhi pamoja na kuchambua,"amesema Bashe.
Bashe amesema serikali imechukua hatua ya kununua vitendea kazi vinavyohitajika kwa maafisa kilimo nchini wapatao 2000 kati ya 7000 hadi kufikia machi 2022 zoezi hilo liwe limekamilika ili waweze kuwahudumia wakulima ipasavyo.
"Tutawapatia pikipiki ambazo tutazifunga GPS na tutawapatia mobile kiti ya kupima udongo ili waweze kuwapatia elimu wakulima juu ya kupanda mazao yanatoendana hali ya udongo wa sehemu husika,"amesema Bashe.
Waziri huyo amesema ili kuondoa dhana ya upotevu wa ardhi ya kilimo wataanzisha sheria na kuhuisha sera ambazo zitaonyesha kila kitu na kuweza kutekeleza hilo anaomba wabunge kusaidia kufanikisha.
Vilevile amesema nanenane itafunguliwa hivi karibuni na maeneo yake yatakuwa vituo ambavyo vitatumika kuwajenga vijana pamoja na kuwaboreshea miundombinu katika masuala ya kilimo.
"Tutashirikiana na serikali za mikoa ambapo Taso katika maeneo ya nanenane tunawashukuru kwa utumishi kutoka tangu mwaka 1993 na sasa hivi maeneo hayo yatasimamiwa na wizara ya kilimo pamoja na sekretarieti ya mikoa na yatakuwa yanafanya kazi mwaka mzima,"amesema Bashe.
Mwenyekiti wa bodi ya Taha, Mhandisi Zebadiya Moshi amesema wanamahusiano mazuri na serikali hali iliyosaidia katika kutatua changamoto karibu asilimia 70 zilizokuwepo katika tasnia ya horticulture kutatuliwa.
"Huu ushirikiano umesaidia kutengeneza mazingira mazuri sana ya uwekezaji katika tasnia hii na tunaamini sana uwekezaji utaendelea kukua kwani Taha tumekuwa tukijitahidi kuelimisha wakulima ili kuongeza tija katika uzalishaji,"amesema Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti huyo amesema pia wamejihusisha na utafutaji wa masoko kwa ajili ya mazao yanayotokana na tasnia hii lengo ni kusaidia mazao ya wakulima kupata soko na kilimo kuongeza thamani.
Aidha amesema kituo cha huduma wa mazoa ya horticulture kilichopo Tengeru toka kuzinduliwa kwake mnamo Octoba mwaka jana kimekuwa na matokeo chanya katika kuwafaidisha wakulima mazao yao kusafirishwa nje ya nchi na kuyaweka katika kiwango cha kimataifa.
Pia amesema kituo hicho kimekuwa ni muhimiri wa kuuza nje ya nchi zao jipya aina ya matango chungu ambapo hadi kufikia januari 28 mashamba yenye jumla ya heka 50 yameshapandwa ambayo yanatoa mavuna zaidi ya tani 350 hivyo wanatemea wakulima watanufaika kupata kiasi cha sh.milioni 440 kwa mauzo yakayofanyika katika kipindi hiki.
Mhandisi Zebadiya amesema pamoja na mafanikio hayo bado kunachangamoto ya nafasi ya usafirishaji wa mazao ya horticulture kwa njia ya ndege pia ongezeko la ufanisi wa bandari katika kusafirisha mazao hayo hivyo ni vyema wakajaribu kuangalia usalama wa mazao.
Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella amesema kilimo ndicho kinachotegemewa katika uchumi wa nchi lakini bado hakijatendewa haki kutokana na hali ya urasimu pamoja na taratibu ambazo si za msingi katika sekta hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPHA,Dk.Ephraem Njau amesema kupitia maelekezo ya waziri watahakikisha wanashirikiana na sekta binafsi kufikia lengo la sekta ya kilimo kukua.
"Kutokana a mamlaka hiyo kushughulika na afya ya mimea pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa viuatilifu kadri ya maagizo ya waziri watahakikisha kilimo kinafikia ngazi ya juu,"alise.a
Alisema kupitia maagizo ya waziri kuwa kunamkakati wa kuwa na ndege ya mizigo ambayo itakuwa inatua katika kituo hicho na kuchambuliwa na kusafirishwa kwenye masoko ya ndani na kimataifa.
0 Comments