Header Ads Widget

RAIS SAMIA ATOA BIL. 1.2 UJENZI DARAJA RUHEMBE

 


Wananchi wa Kata ya Ruhembe Wilaya ya Kilosa Mkoa Morogoro wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia kiasi Cha shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja katika eneo hilo.


Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa eneo Hilo Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mheshimiwa Lazaro Londo amesema endapo Daraja Hilo litakamilika kwa wakati litainua uchumi wa wananchi wa Kata hiyo na Kata jirani .


Londo anasema  watu kadhaa wamekufa maji wakati wakijaribu kuvuka mto huo hivyo wanamshukuru Rais Samia kwa fedha hizo alizowapatia 


Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilosa  Mhandisi Harold Sawaki  anasema tayari wamemkabidhi mkandarasi aliyefahamika kwa jina la  Kampuni ya Famost Company Ltd eneo la ujenzi wa Daraja kubwa la Ruhembe



 Zawadi Anasema  Daraja hilo litakua na ukubwa   mita 40 na upana mita 9.84 na kinatarajia kukamilika kwa kipindi Cha miezi mitano


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majd Mwanga amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha kwa wakati ujenzi wa Daraja Hilo 


DC Mwanga anasema Rais Samia licha ya kutoa kiasi Cha shilingi Bilioni 1.2 ujenzi wa Daraja la Ruhembe lakini  pia ametoa zaidi ya shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Berege wilayani humo



Shughuli hiyo  pia imehudhuriwa na viongozi wa chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilosa   wakiongozwa na katibu wa ccm wilaya  Shaban Mdoe ambapo  amesema uujenziwa daraja Hilo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM)


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI