Header Ads Widget

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWAKA ULIOISHIA 2021 WAONGEZEKA

  



Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2021 umeongezeka kidogo kwa pointi za asilimia 0.1 kutoka asilimia 4.1 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2021 na kufikia asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba.


Hayo yameelezwa  Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Makazi kutoka NBS,  Ruth Minja wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokua akitoa takwimu za mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia 2021.


Aidha, amesema kuongeza kwa mfumuko huo wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2021 kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Disemba 2021 zikilinganishwa na bei za mwezi Disemba 2020.


"Kasi hii inamaanisha kuwa mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2021 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2021"amesema Minja


Akitaja baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi Desemba 2021 zikilinganishwa na bei za mwezi Desemba 2020 ni pamoja na mchele asilimia 2.6, unga wa mtama 2.8, nyama ya ngombe 6.4, nyama ya mbuzi 8.3, mayai 4.8, Viazi 5.3 pamoja na vinywaji baridi 5.1.


Kwa upande upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei mwezi Desemba 2021 amesema ni pamoja na vinywaji vikali na tumbaku kwa asilimia 2.2, mavazi na viatu 4.5, Kodi ya pango 4.4, vifaa vya Ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za makazi 7.7, Gesi 5.5, mkaa 3.4 , mazulia 9.2, huduma za Usafirishaji wa abiria kwa njia ya reli na Barabara 3.9, huduma za chakula na vinywaji kwenye migahawa 4.7 pamoja na huduma za malazi kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni 6.6.


Hata hivyo amesema Mfumuko wa Bei za bidhaa za vyakula ma vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2021 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.9 kutoka 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2021.


" Kwa upande mwingine Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi bidha za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Desemba 2021 umepungua hadi asilimia 3.9 kutoka 4.0 ikivyokuwa kwa mwaka ulioishia Novemba 2021"amesema Minja


Minja alibainisha kuwa Mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula visivyochakatwa yaani Nishati, na bili za maji kwa mwezi Desemba 2021 umepungua hadi kufikia asilimia 4.6 kutoka asilimia 4.7 ilivyokuwa mwezi Novemba 2021.


Akizungumzia kuhusu Fahirisi za bei  za Taifa , amesema zimeongezeka kutoka 100.73 mwezi Desemba 2020 hadi kufikia 104.92 mwezi Desemba 2021.


Amesema kuwa, kuongeza kwa Fahirisi kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.


Hata hivyo, amesema baadhi ya bidhaa hizo ni mchele asilimia 3.7, mahindi 5.2, unga wa ngano 3.4, unga wa mahindi 3.3, Vyama ya ngombe 2.3, nyama ya mbuzi 1.6, samaki 5.3, matunda 3.7, mbogamboga 2.3 pamoja na viazi 3.2.


Aidha amesema kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia ni pamoja na vifaa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za makazi asilimia 5.0, gesi 2.3, mafuta ya taa 1.7, diseli 6.7, petroli 3.0

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS