Header Ads Widget

MBUNGE NDAKIDEMI ATAKA WANANCHI KUSHIRIKISHWA FEDHA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI YAO.




NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

MBUNGE wa jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi amesema kuwa serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo lakini wananchi wamekuwa hawatambui kutokana na miradi hiyo kutosemewa.



Prof. Ndakidemi alitoa kauli hiyo jana katika kikao cha Baraza maalum la madiwani wa halmashauri ya Moshi kujadili utekelezaji wa bajeti ya Wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) pamoja na wakala wa maji (RUWASA) kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na bajeti yam waka mpya wa fedha 2022/2023.


Mbunge huyo alisema kuwa, kwenye upande wa barabara serikali imetoa Bilioni 1.5 kila jimbo ambapo Bilioni 1 imetokana na fedha za tozo lakini wapo wananchi hawatambui fedha hizo zimetumikaje.



"Watekelezaji wa miradi hii inayotolewa na serikali mnajukumu kubwa la kuhakikisha kila mnapokwenda washirikisheni viongozi wa vijiji, kata na wilaya ili wao wawe na jukumu la kuisemea miradi hii kwa wananchi watambue serikali yao inafanya nini" alisema Prof. Ndakidemi.


Mbunge huyo alisema kuwa, kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watendaji wa serikali wanaotekeleze miradi kutoshirikisha viongozi wa serikali za wananchi hali inayopelekea kuona miradi ikitekelezwa bila kutambua kuwa fedha za utekelezaji wake zimetoka serikalini au kwa wafadhili.



Alisema kuwa, endapo wananchi watashindwa kujua serikali yao imetoa fedha kutakuwa hakuna kitu kinachofanyika na inawezekana kuwachonganisha viongozi na wananchi.

Mwisho....

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI