Header Ads Widget

BEKI AXEL TUANZEBE AISHTAKI MAN UTD

 

Beki wa zamani wa Man United Axel Tuanzebe

Beki wa zamani wa Manchester United Axel Tuanzebe ameishtaki klabu hiyo kwa madai ya ushauri mbaya wa kimatibabu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye alijiunga na Burnley mapema mwezi huu, aliwasilisha madai ya kisheria katika Mahakama Kuu dhidi ya United wiki iliyopita.

Inahusiana na kipindi cha kuanzia Julai 2022 kinachohusisha jeraha lisilojulikana na inachukuliwa kuwa dai la thamani ya juu, ambalo linaeleweka kuwa zaidi ya £1m.

Tuanzebe alikuwa nje kwa siku 195 katika msimu wake wa mwisho katika klabu hiyo kabla ya kupelekwa kwa mkopo katika timu ya Stoke Januari 2023, ambako alicheza mechi tano pekee.

Alijiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka minane, akicheza mechi yake ya kwanza mwaka wa 2017, na aliichezea mara 37 kabla ya kuondoka msimu wa joto wa 2023, akijiunga na Ipswich kama mchezaji huru Septemba hiyo.

Beki huyo wa kulia alikuwa nahodha wa United katika kila ngazi na mechi yake ya mwisho kuichezea klabu hiyo ilikuwa fainali ya Ligi ya Europa 2021 dhidi ya Villarreal, ambapo alifunga kwenye mikwaju ya penalti walipopoteza kwa mikwaju 11-10.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21 - ambaye sasa anaiwakilisha DR Congo - pia alikuwa na misimu mitatu kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa, huku pia akiwa Napoli mwaka 2022.

Mawakili wa Tuanzebe, Simons Muirhead Burton, na United wote walikataa kutoa maoni yao walipoulizwa na BBC Sport.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI