KADA wa chama cha mapinduzi (CCM) aliyewahi kuwa mkuu wa Wilaya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdallah amerejesha fomu za kuomba kuwania uspika kupitia CCM .
Asia amerejesha fomu hiyo kwa mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi CCM, Cuthbert Midala katika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma Januari 14,2022.
Hadi tarehe 14 jumla ya wanachama wa CCM 66 wamechukua fomu ya kuomba kuwania nafasi hiyo hiyo iliyoachwa wazi na Job Ndugai aliyejiuzulu nafasi hiyo ikumbukwe mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Januari 15, 2022.
0 Comments