Header Ads Widget

JIJI LA DODOMA LAENDELEA NA ZOEZI LA USAFI .

 



Na Hamida Ramadhan Dodoma 


JIJI la Dodoma limeendelea na zoezi la ufanyaji wa usafi kwenye Kata na Mitaa yote ya jiji ambapo Mkurugenzi wa Jiji hilo Joseph Mafuru akiahidi kutuma kikosi kazi cha kuhakikisha mapangale ya muda mrefu yanaondolewa na vichachoro vyote vinakuwa safi.


Amesema hayo leo jijini hapa wakati wa zoezi la ufanyaji wa usafi katika Kata ya Kikuyu St John ambapo amesema  mapangale na vichochoro vimeonekana vikificha vichaka na uchafu .


"Jumatatu itakuja Team yangu kutembea tena hapa katika kata ya Kikuyu ili kuona viwanja gani vina mapagale  ya muda mrefu na ambavyo vinavichaka na uchafu wa muda mrefu ,"amesema 


Na kuongeza kusema kuwa "Nakwanini tunakuwa na mapagale ya muda mrefu katika jiji letu kwani hata katika Hati kuna sheria inayosema pagale kwa muda wa miaka mitatu liwe nimekwisha jengwa,"amesema Mkurugenzi Mafuru.



Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri amesema usafi unaepusha maradhi hivyo ni wajibu wakila mwanachi kujitafakari na kujituma katika zoezi zima la ufanyaji wa usafi katika eneo linalomzunguka.


Aidha kwa upande wa kufunga maduka siku ya Jumamosi amesema watakaa na kuliangali hilo kwa undani zaidi kwani imebainika wananchi wengi hasa wafanyabiasha wamekuwa wakifunga maduka na kwenye zoezi la usafi hawafanyi.


"Nitakaa na team yangu kuliangalia hili suala la kufunga maduka siku ya Jumamosi kwa mfano maduka ya dawa  hatuwezi kufunga maduka wakati wengine wanahitaji kupata dawa huku watu wamefunga maduka na hata kwenye zoezi zima la usafi hawashiriki tutakuja na hatua nyingine nzuri ya kuwashirikisha watu kufanya usafi ," Shekimweri .


Naye Diwani wa kata hiyo Israel Mwasansu amesema suala la usafi ni endelevu kuanzia kwenye kaya mpaka kwenye jumuiya na kuendelea kusema suala la usafi ni ustarabu wa mtu hivyo kila mmoja ajitoe kufanya usafi maeneo yanayonzunguka ili kuhakikisha jiji la Dodoma linakuwa safi na la kupendeza.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI