Isimila ni eneo la kihistoria lililopo katika kijiji cha Ugwachanya, kata ya Mseke, wilaya ya Iringa mkoani Iringa kusini mwa Tanzania, kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya Iringa – Mbeya
Njia ya kuingia si rahisi kuikuta:
ukitokea Iringa iko kabla ya kufikia Tanangozi, upande wa kushoto,Eneo hili
ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa
wa Iringa.
Bonde la Isimila
lilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe za Kale Ni katika eneo hilo ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila
zilipogunduliwa tangu mwaka 1951.
Zana
hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka 260,000 kabla ya
Kristo, umri uliopatikana kwa kupimwa mifupa ya
kibinadamu iliyokutwa kati ya mawe yaliyochongwa kama zana
Miongoni
mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila, ambalo lina mikondo
miwili, ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe
ya kombeo kwa ajili ya uwindaji.
Korongo la pembeni lina mmomonyoko wa ardhi ulioacha nguzo za
ajabu.
Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa
zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zana nyingine na shoka zilizotumika
kwa kazi ya
kuvunja mifupa, nyembe na visu.
Pia
ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi
vimeonekana; kati yake ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na ya twiga wa hivi sasa,
ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi,
ambapo pia kulikuwa na aina tofauti ya viboko.
Kumbuka utalii ni moja kati ya nguzo ya uchumi wa Tanzania na tayari serikali imekuwa ikiwekeza nguvu nyingi zaidi katika kutangaza utalii japo kasi ya watanzania kutembelea vivutio vya utalii ni ndogo sana ukilinganisha na wageni wanaofika katika kutalii kutoka nchi mbali mbali duniani .
0 Comments