Ikiwa leo ndio zoezi la kuhitimisha uchukuaji na urejeshaji wa fomu ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Chama Cha Alliance For Democratic Change( ADC), Mgombea pekee wa chama hicho Maimuna Saidi amerejesha fomu aliochukua Januari 16 makao makuu ya Chama jijini Dar es salaam........Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Akizungumza mara baada yakukabidhi fomu hiyo, kwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara wa ADC, Maimuna amesema, ameamua kugombea nafasi hiyo kwa sababu ana sifa za kuliongoza bunge hilo, na endapo atateuliwa na Chama chake nakuweza kushinda nafasi ya Usipika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha anaunganisha mihimili ya serikali ambayo ni Mahakama,Bunge na Serikali ili ifanye kazi kwa ushirikiano.
"Nina haki yakikatiba kugombea nafasi hii ya Uspika,pia nitahakikisha Bunge linakua na ushirikiano na mihimili mingine ili ifanye kazi kwa pamoja kwa kufuata haki sawa katika kusimamia, kukosoa na kushauri serikali" amesema Maimuna.
Kwa upande wake, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Doni Mnyamani amesema hadi sasa ni mwanachama mmoja wa chama hicho ndio amejitokeza kuchukua fomu yakuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kikao cha kamati tendaji ya Chama hicho kinatarajiwa kuketi Januari 20 kwa ajili yakupitisha jina la mgombea mmoja ili lipelekwe Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
"Leo ikiwa tunahitimisha zoezi hili, mgombea pekee wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Maimuna Saidi amerudisha fomu mbayo alichukua jumapili ya tarehe 16 kwa ajili ya Kuomba kugombea nafasi ya Usipika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya aliyekua Spika wa Bunge hilo Job Ndugai kujiuzulu, mpaka sasa tuna mtu mmoja tu aliejitokeza kuchukua fomu " amesema Mnyamani
Hata hivyo, amesema kuwa tarehe 20 mwezi huu, kamati tendaji ya ADC itakutana kupitisha jina la mgombea mmoja kati ya wale watakaojitokeza kuchukua fomu na jina hilo kulipeleka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya taratibu zingine, lakini tunaendelea kupokea wengine watakaopenda kuja kuchukua fomu.
0 Comments