Header Ads Widget

WATANZANIA WAZIDI KUNUFAIKA NA PROMOSHENI YA TIGO WAJIFTISHE GIFT JUU YA GIFT

 Na Mwandishi Wetu.

Ikiwa ni wiki ya pili tangu kuanza kwa kampeni ya WAJIFTISHE GIFTI JUU YA GIFTI inayoendeshwa  na Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania Kijana EZRA MWAIKAMBO mkazi wa Kiwalani Dar es salaam ameibuka mshindi baada ya kujinyakulia pikipiki aina ya Boxer kupitia KAMPENI YA TIGO "WAGIFTISHE  GIFT JUU YA GIFT".



Akielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa pikipiki mshindi huyo ameishukuru Tigo kwa kuwajali wateja wake huku akieleza matarajio yake kuwa ataenda kuanzisha biashara ya usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda na hivyo kumuwezesha kujiajiri yeye mwenyewe na hivyo kujikwamua kiuchumi.



Akimpongeza mshindi wa pikipiki hiyo pamoja na washindi waliojishindia simu janja Meneja wa Tigo kanda ya Pwani,Kaskazini, ROBERT KASUGA amesema katika mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidijitali nchini, kampuni ya Tigo imewahakikishia wateja wake kuwa kila mtu anapata nafasi ya kumiliki simu bora ya kisasa kwa bei nafuu zaidi kwa kila ununuzi wa simu za kisasa za ITEL T20 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote, hivyo akawaomba wateja waendelee kununua simu za ITEL T20 kutoka maduka ya Tigo nchini kote ili kuingia kwenye droo ya kupata nafasi ya kujishindia moja ya pikipiki kati ya 5 zikiwemo simu janja zinawaniwa katika promosheni hiyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI