Katika kutatua changamoto za kimaisha sambamba na kupanua wigo wa kukua kiuchumi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa wananchi wametakiwa kutumia vyema fursa zinazotolewa na taasisi za fedha ikiwemo vyama vya kuweka na kukopa yaani saccos........Na Gift Mongi Moshi Kilimanjaro
Hatua hiyo imetajwa kuwa ni sehemu sahihi na salama katika kujenga uwezo na matumizi sahihi ya fedha ambapo pia huweza kuchangia kukuza mitaji kwa wafanyabiashara au hata wajasiriamali wadogowadogo.
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi alitoa rai hiyo mara baada ya kukabidhi msaada msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa chama ushirika wa akiba na mikopo cha Umoja Saccos iliyopo kata ya Kimochi wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
"Chama hiki kwa kipindi kirefu kimekuwa na ukaribu na ofisi yangu hivyo nami nikaona no vyema kuwaunga mkono kwa huu ujenzi unaoendelea lengo ni kutoa wigo kwa wananchi kujikwamua kiuchumi"alisema
Alisema mbali na kukabidhi mifuko 50 ya saruji,mchanga pamoja na fedha za ufundi vikiwa na thamani ya milioni 1.4 bado ataendelea kuongeza nguvu kwenye ujenzi huo kadri fursa zitakapojitokeza kwani ni taasisi muhimu kwa watu ambao hawataweza kupata huduma kwenye taasisi kubwa za kibenki.
Kwa upande wake meneja wa chama hicho Kulwa Mgeni mbali na kumshukuru mbunge huyo kwa msaada wa vifaa hivyo amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutaenda kuongeza ufanisi nanwigo mpana katika kuwahudumia wananchi.
" Kumalizika kwa ujenzi wa jengo hilo kutarahisisha huduma za kibenki pamoja na zile za chama kwa wanachama na wananchi wa eneo hilo tofauti na sasa na kuwa lengo ni kuwafikia wananchi wengi zaidi"alisema
Naye diwani wa Kata hiyo ya Kimochi Ally Badi alisema ni hatua muhimu inayopaswa kuungwa mkono na wadau wa maendeleo ili kufikisha huduma za kifedha karibu na wananchi.
0 Comments