WANANCHI wametakiwa kuepukana na utumiaji wa dawa kiholela kwani utumiaji madawa holela usababisha madhara makubwa kwa afya ya binadamu.....Na Hamida Ramadhan Dodoma
Mbali na kuwataka wanachi kutokutumia dawa kiholela wametakiwa kutonunua madawa katika maduka ya madawa muhimu ya binadamu ambayo hayajasajiliwa na baraza la Famasi .
Hayo yameelezwa na Msajli wa Baraza la Famasi Elizabeth Shekhalaghe alipokuwa akizoa taarifa ya kwa Umma kuhusu matumizi holele ya dawa.
Sambamba na hayo wamiliki wote wenye wenye maduka ya dawa wanatakiwa kuhusha leseni zao ambapo mwisho wa kuhuisha ni Desemba 31 mwaka huu vinginevyo wasiofanya hivyo watafutiwa leseni.
Amesema kuwa pia ni marufuku mmiliki wa duka la dawa kuweka matangazo ya kujitangaza na kwa kuweka mabango ya matangazo matangazo ni kosa kisheria.
Ameeleza kuwa kutokana na majukumu ya Baraza la Famasi wananchi wanapaswa kuelewa kuwa dawa ni nini na matumizi sahihi ya dawa ni nini ili kila anayetumia basi aweze kuelewa umuhimu huo na athari zake.
"Kwa kifupi, dawa ni kemikali au kitu chochote kinachotumika kutibu, kuzuia au kutambua magonjwa ya binadamu au wanyama.
Amesema matumizi sahihi ya dawa yanajumuisha mgonjwa kufanyiwa uchunguzi wa kina, kuandikiwa na kupewa dawa inayostahili kulingana na hali ya ugonjwa alionao kwa kutumia kiasi sahihi, kwa njia sahihi na kwa muda muafaka kama alivyoelekezwa na mtaalam wa afya.
"Nitoe wito kwa wananchi kutambua kwamba Dawa ni sumu na huleta madhara iwapo hazitatumika ipasavyo hivyo ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na ushauri wa wataalamu kwa matokeo mazuri ya tiba za magonjwa yanayowakabili," amesema
0 Comments