Header Ads Widget

VIJANA WA CCM KAGERA WAAHIDI KUENDELEA KUMLINDA NA KUMSEMEA DKT. SAMIA

 


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Burhan, ameahidi kuwa vijana wa Jumuiya hiyo  watamlinda na kumsemea kwa wivu mkubwa mgombea wa nafasi ya  urais kupitia Chama cha  Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa vijana hawatakubali kushawishiwa kujiingiza kwenye vitendi vya  uvunjifu wa amani.



Akizungumza   katika mkutano wa kampeni wa mgombea nafasi ya Urais kupitia Chama cha Mapinduzi  Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Viwanja vya Kaitaba, Bukoba Mjini mkoani Kagera, Burhan amesema vijana wa CCM watakuwa mstari wa mbele kuzitafuta na kuzilinda kura za ushindi wa Dkt. Samia kwa amani na umoja.


Burhan ameeleza kuwa dhamira hiyo imetokana na mafanikio makubwa ya Dkt. Samia katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, ambayo imekuwa suluhisho kwa changamoto za vijana nchini, ikiwemo upatikanaji wa ajira na fursa za kiuchumi.


Akitolea mfano Mkoa wa Kagera, Burhan amesema serikali ya awamu ya sita imetekeleza kwa vitendo sera za uwezeshaji wa vijana kiuchumi, ambapo takribani Shilingi bilioni 15 za mikopo zimetolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu — ongezeko kubwa kutoka bilioni 3.2 zilizokuwa zinatolewa kabla ya uongozi wa Dkt. Samia.


Burhan amemuelezea Dkt. Samia kama “Mwalimu wa siasa za kikomavu”, akisema kampeni zake zimekuwa kielelezo cha ustaarabu, uvumilivu na siasa za hoja, jambo ambalo limevutia vijana wengi ambapo wamedhihirisha kuwa October 29 watampigia kura za kishindo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI