Halmashauri ya Arusha iliyopo wilayani Arumeru imeendelea na jitihada za ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ambapo hadi sasa umefikia asilimia 95 nakutarajiwa kukabidhiwa mnamo Desemba 15 kutokana na maagizo ya serikali.....Teddy Kilanga Arusha
Akizungumza na Matukio Daima leo ofisi kwake,Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Suleiman Msumi alisema kupitia fedha za uviko takribani sh.bilioni 2 kwa ajili ya madarasa 96 yamejengwa katika shule za sekondari 30.
Aidha Msumi alisema madarasa manne kutoka katika shule za msingi shikizi ambapo inatengeza takribani sh.bilioni nne za jumla ya fedha za uviko walizopatiwa na serikali kwa ajili ya madarasa 100 ambapo inakamilisha idadi hiyo katika ujenzi wote.
"Hivyo tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendeleo wa kutupatia fedha za ujenzi wa madarasa kwani hapo awali iliwaladhimu wananchi kuchangishana fedha kwa ajili ya ujenzi vyumba vya kusomea watoto wetu,"alisema Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo.
Msumi alisema hadi sasa wako katika asilimia 96 ya ujenzi wa madarasa yote 100 kwani kupitia fedha hizo zilizoelekezwa katika vyumb vya madarasa wananchi wamenufaika kwa njia mbalimbali ikiwemo ajira za muda ziliongezeka.
"Ukiangalia fedha hizi zimeweza kuondoa kero ya kila mwaka ya ujenzi wa madarasa ambapo hali ilikuwa ni changamoto kwao hivyo Rais Samia ameweza kuwatua mzigo huo wananchi,"alisema.
Aliongeza kuwa anashukuru huwepo wa ushirikiano kati ya madiwani,wataalamu na wananchi,walimu wakuu pamoja na watendaji wa kata na vijiji katika kufanikisha ujenzi huo kufikia katika asilimia hizo.
Hata hivyo alisema kati ya hayo madarasa 100,ishirini na nne yapo katika mijengo ya ghorofa ambayo nayo yapi katika hatua za ukamilishwaji.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Laroi ,Ojung'u Salekwa alisema hawana maneno sahihi ya kumshukuru Rais wa Samia kwani amesaidia kuondoa upungufu wa madarasa katika kata mbalimbali.
"Kata ya Laroi madarasa manne pamoja na nyinginezo kwani ametusaidia sana kwasababu ameondoa changamoto za kuchangishana na wananchi fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hali hiyo haitakuwepo tena nchini mwetu,"alisema Mwenyekiti.
Mwenyekiti huyo alisema mapokeo ya ujenzi madarasa wananchi na viongozi mbalimbali wamepokea kwa mikono miwili na kuhakikisha katika ule muda ambao serikali umetenga kufikia Desemba 15,2021 watakuwa wamekabidhi kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi.
Salekwa alisema kuna baadhi ya maeno kam kata ya Mateves wameshakabidhi madarasa yakiwa na samani zote.
0 Comments