Header Ads Widget

TANAPA YAWATUNUKU 'WAGUMU' MLIMA KILIMANJARO...

 





Hamali/mpagazi/mchukuzi ni maneno yenye maana sawa yakimaanisha mtu ambaye anabeba mizigo kwa malipo..........Na Gift Mongi_Kilimanjaro



Ingawa katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro watu hawa wapo na wamekuwa wakitoa huduma hii kwa watalii kwa kipindi kirefu na sasa wamebatizwa jina lingine la 'wagumu'.




Wapagazi 'wagumu' wamekuwa na msaada sana kwa watalii pindi wanapoenda kufanya matembezi na ni dhahiri kuwa shughuli zinazofanyika katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro bila uwepo wao ingekuwa ni kazi ngumu Sana au hata isifanyike kama ilivyokusudiwa kutokana na ugumu wenyewe.





Katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika watu 152 walipandisha bendera juu ya kilele Cha mlima Kilimanjaro safari ambayo ndani yake iliwezeshwa kwa kiasi kikubwa na wapagazi 'wagumu'zaidi ya 200.




Katika safari hiyo jumla ya watu 79 waliweza kufika katika kilele cha uhuru chenye urefu wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari huku wengine wakiishia njiani kutokana na mambo mbalim ali zikiwemo sababu za kiafya.





Kutokana na kazi hiyo kufanyika kwa ustadi mkubwa na mafanikio hatimaye bodi ya  wakurugenzi ya Mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA), ikatoa  zawadi ya Milion 5 .




Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TANAPA Jenerali mstaafu George Waitara alitoa tamko hilo la kuwapongeza wapagazi 'wagumu' hao wakati wa hafla fupi ya kupokea msafara huo ulioongozwa na Kanali Martin Msumari wa JWTZ.




" Wagumu wanafanya kazi ngumu Sana na mkumbuke kupanda Mlima Kilimanjaro ni kazi ngumu sana ila wao mvua inyeshe jua liwake wanahakikisha mambo yanaenda sawa kwa kuhakikisha wapanda mlima wanafika kileleni leo nawapongeza kwa zawadi ya milioni 5"Alisema




Alisema katika maadhimisho ya mwaka huu 2021 amefurahishwa na wajumbe wawili wa bodi ya TANAPA waliojitokeza kupanda Mlima Kilimanjaro na kujionea mandhari nzuri ya Mlima huo, lakini pia menejimenti ya Tanapa litasaidia wakati wa kufanya maamuzi mbalimbali kuhusiana na uboreshaji wa Mlima huo.




Waitara pia alisema amepokea maoni ya wadau kuhusu wageni wanaopanda mlima Kilimanjaro  kupewa ngao (kidani),  mbali na cheti ili kulivaa wakati wote na kuonyesha alama ya kupanda mlima huo  hivyo amewaachia menejimenti ya TANAPA kutafakari hilo na kuona namna ya kulifanikisha.




Aliishukuru kampuni ya utalii ya Zara Tours Kwa kufanikisha zoezi la kupandisha wageni 150 katika Mlima Kilimanjaro na kusema pamoja na kwamba hiyo ni safari ya kwanza katika historia kuwa na wageni wengi lakini kampuni hiyo imeweza kufanikiwa.




" Wageni 150 sio jambo la mchezo kabisa lakini tumeshuhudia wafanyakazi wa kutosha kuanzia waongoza watalii(guides) na wapagazi (wagumu ) wa kutosha ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kuhakikisha  wageni wote wanapanda mlima bila kikwazo, niseme tu hongera sana kwa Zara ikiongozwa na Mama Zara kama ambavyo tumezoea kukuita," alisema Waitara.




Kanali Msumari alikabidhiwa Bendera ya Taifa Disemba5, mwaka huu na Naibu Spika Tulia Ackson na kutakiwa kuongoza watanzania 150 na kuiweka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kumbukizi ya miaka 60 ya Uhuru




Msafara huo uliojumuisha watu kutoka maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wanajeshi, waandishi wa habari, watendaji katika taasisi za Serikali na binafsi ulianza safari Desemba 5,mwaka huu kwenye geti la Marangu majira ya saa saba mchana na wapandaji kukamilisha siku ya kwanza katika kituo cha Mandara.




Safari hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa, (TANAPA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Uwakala wa Utalii ya ZARA siku ya pili wapandaji walitembea hadi katika kituo cha Horombo  na kukaa kwa siku mbili na siku ya nne walitembea hadi katika kituo cha Kibo  umbali wa Kilometa 11 kabla ya siku ya tano usiku wa saa5 kuamkia Disemba 9, 2021 kuanza kupanda kilele cha Mlima Kilimanjaro. 





Kwa upande wake kiongozi wa msafara huo Kanali Martin Msumari alisema hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Shirika la TANAPA na kampuni ya utalii ya Zara kwa pamoja zimeweza  kuandika historia kubwa  kwa mara ya kwanza wapandaji150 wamepanda mlima Kilimanjaro.




Alisema katika safari hiyo wapandaji mlima 79 walifanikiwa kufika kilele cha Uhuru ikiwa ni historia ya kwanza katika mlima huo kwa idadi kubwa sana kufika kilele hicho cha urefu wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.




Kanali Msumari alisema waliopanda hadi kituo cha Stella kituo kimoja kabla ya kufika kilele cha Uhuru  walikuwa wapandaji 3, Gilmans p 5, na waliotembea hadi eneo la Kibo walikuwa 30, Horombo 20 na Mandara 8.




Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye alikabidhiwa Bendera na Kanali Msumari, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kigaigai alisema Mlima Kilimanjaro unapaswa kulindwa kwa ushirikiano wa watu wote kwa kuwa ni hazina kubwa ya hifadhi ya uoto wa asili na maji yake yamekuwa chanzo kikubwa cha uhai wa wakazi wa kanda za kaskazini na Mashariki


"Nilipofika hapa Kilimanjaro kaka Mkuu wa Mkoa nilitembelewa na Mhifadhi wa Kinnapa Angela, alinieleza mambo mengi kuhusu Mlima, tangu siku hiyo niliamua kuwa balozi wa mlima huu kwa kuwa ndio unaopeleka maji mto pangani na nyumba ya Mungu na kutumika kuzalishia umeme lakini pia shughuli za umwagiliaji huko chini wanatumia maji haya lakini pia matumizi ya kawaida maji yake yote yanatoka hapa,"Alisema Kigaigai.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI