Header Ads Widget

SHULE SEKONDARI YA WASICHANA ARUSHA YAIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA SAYANSI BIASHARA.

 





Shule ya sekondari ya wasichana Arusha imeibuka mshindi katika shindano la sayansi biashara yaliyokuwa yakishindanisha bunifu mbalimbali za kisayansi ambazo pia zinaweza kuwa biashara na kutatua changamoto katika jamii......NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA



Baadhi ya wasichana wa shule hiyo wa kidato cha tano wameshinda baada ya kufanikiwa kugundua kifaa cha kisayansi cha kuua wadudu katika mimea ambacho kitasaidia wakulima kutumia kuuwa wadudu katika mashamba pasipo kutumia kemikali zitakazoweza  kuathiri afya udongo na afya za walaji.



“Tulifanya tafiti kupitia wataalamu mbalimbali ambapo tulibwini kabaini changamoto ya matumizi ya kemikali katika kuua vijidudu katika mazao na wakulima wengi kutojua matumizi sahihi  ya viuatilifu na teknolojia hii tuliyoibuni inaua wadudu bila kugusa mmea,”Alisema mmoja wa wanafunzi hao kutoka shule ya Sekondari ya wasichana Arusha




Walisema kuwa kifaa hicho kinatumia  harufu kuwavuta wadudu kuingia ndani ambapo baada ya kuingia  wanakutana na mafuta ya mmea wa mwarobaini ambayo yanawangamiza  na kusema kuwa njia hiyo ni bora kwani haina madhara kwa mkulima mwenyewe, mlaji lakini pia ardhi.




Kwa upande wake Kaimu mkuu wa chuo cha ufundi Arusha Dkt Mussa Chacha ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika mashindano hayo  alisema kati ya eneo walioshindwa kwa miaka mingi ni elimu ya sayansi kuiunganisha na biashara ni vyema  wanafunzi hao wakatilia mkazo katika  eneo hilo la kuwa wabunifu katika kuvumbua vitu vya kisayansi ambavyo vitakuwa ni biashara lakini pia vitakavyosaidia jamii.





Naye Josephine Sepeku meneja wa mradi huo wa kuwasaidia wanafunzi wabunifu kubuni tafiti zitakazo tatua changamoto katika jamii  alisema kuwa mashindano hayo yakianza mwezi wa sita na sasa katika fainali ambapo wamepata mshindi  ambaye ameweza kuonuesha bunifu yao ya kutatua changamoto inayoikabili sekta ya kilimo.


Alisema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na tija  wanafunzi kwani wanafunzi wamefanya sayansi ya vitendo kuilinganisha pamoja na biashara ili kutatua changamoto katika jamii pamoja na kujiingizia kipato ambapo shule zilizoingia kwenye mashindano hayo ni pamoja na Arusha Sekondari,Ilboru ,Edimund Rice,Bishop duning na Arusha girls ambapo.



Mmoja wa walimu Exaudy Mollela amewaomba wadau kujitokeza katika kuwekeza katika mawazo ya bunifu hizo ili kupanua wigo wa matumizi ya kifaa hicho kwani hawana vyanzo vya kutosha vya mapato

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI