WASANII wa kizazi kipya Mkoani Njombe wamelalamikia kitendo cha Wanasiasa kuwatumia kipindi cha kampeni na kuwatelekeza kwa kuwapa ahadi hewa.........Na Frederick Siwale - Mdtv Njombe.
Akizungumza na Matukio daima tv Msanii Stanley Mgaya a.k.a B.Alone alisema imekuwa jadi kwa wanasiasa kuwatumia wasanii kipindi cha kampeni za kisiasa na matukio ya Kitaifa kwa upande wa Serikali kwa kulipa ujira mdogo na kuadi kede kede ambazo huwa hazitekelezeki hadi kampeni nyingine au matukio ya Kiserikali.
" Mwandishi imenibidi nifunguke kwa niaba ya wasanii wenzangu wa mkoa wa Njombe ,kwani tumegeuzwa kama tambala la kudekia ambalo likisha tumika na thamani yake inakuwa imeishia hapo hadi litakapo hitajika" Alisema Mgaya.
Alisema tangu ameanza sanaa ya nyimbo za bongo fleva ni zaidi ya miaka 15 lakini anaishia kupewa sh.50,000 au sh.200,000 wakati kazi kama zake na za wengine Njombe zinafanana na Wasanii wa Jijini Dar es salaam ambao wao wakifika wanalipwa kuamzia sh.300,000,000 hadi milioni 5 .
"Wakati wasanii wenzetu wanakula maisha sisi Njombe tunaishia kuambiwa baada tukio hili nitakuendeleza kielimu na kukutafutia vifaa vya muziki miaka nenda rudi" Alisema Mgaya.
Mgaya alisema tatizo ni Wanasiasa na Viongozi wa Serikali kutothimini mchango wa Wasanii wa nyumbani na kuamini kuwa Wasanii wa kubwa ni kutoka katika majiji makubwa .
" Mwandishi ni kama dharau tunafanyiwa bila kufahamu kuwa wasanii huku tunaonekana wachanga kila kukicha ili hali hata huko Waliko wasanii wakubwa baadhi ya wacheza show wao wanatokea huku.
Kuaminisha kuwa mikoani wanaweza Mgaya alisema kuna mcheza show mmoja yupo na kundi la msanii mkubwa sana aitwaye Angel Nyigu na anafanya vizuri ,mbona hapuuzwi kama tunavyo puuzwa sisi ? Alihoji Mgaya.
Hivyo Mgaya B.Alone alisema umefika wakati kwa Wanasiasa kuona upo umuhimu wa kuwajali na kuwatimizia ahadi zao badala ya kuwageuza matambala ya deki ambayo hutumika kwa wakati na yakisha tumika yanaonekana ni uchafu sawia na Serikali kuona umuhimu wa kuwajali wakati ungalipo.
0 Comments