Header Ads Widget

NGOME YA WANAWAKE ACT WATOA MSAADA TUNDURU

 




Katibu wa Kikosi Kazi Cha Ngome ya Wanawake Taifa Wakili Bonifasia Mapunda leo Desemba 7, 2021 amefanya kikao na Viongozi wa Ngome ya Wanawake Jimbo la Tunduru Kaskazini mkoani Ruvuma.


Kikao hicho kilichofanyika katika  Kata ya Muhuwesi kilifunguliwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu Ado ambaye pia  amepata kuwa Mgombea Ubunge wa jimbo hilo mwaka 2020. 



Akizungumza na Wanawake hao, Wakili Bonifasia amewashukuru Wanawake wa Kata ya Muhuwesi na Jimbo la Tunduru Kaskazini kwa ujumla kwa mchango wao wa hali na mali wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 na kuwataka kuendelea na mapambano ya kujenga chama huku akiahidi kuwa chama kitaendelea kuwa nao begabega katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake na jamii kwa ujumla. 


Aidha katika tukio hilo, Wakili Bonifasia kwa niaba ya Ngome ya Wanawake alikabidhi mabeseni 100 ya kuwasaidia wazazi kwenye Zahanati ya Muhuwesi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI