Mameneja waandamizi wa Tanesco pamoja na wafanyakazi wa Tanesco Kanda Ya Kaskazini wamepewa elimu ya kuelimishwa kanuni na taratibu za ufanywaji wa kazi ili kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali ya awamu ya sita yanatimia na kazi za umeme zinafanywa kwa kuzingatia kanuni na Sheria.
Akizungumza na katika semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA) Meneja wa mamlaka hiyo Kanda ya kaskazini Lorivi Long'idu amesema kuwa elimu itakayotolewa kwa wadau hao itasaidia kumaliza changamoto zilizopo na kuboresha zaidi huduma.
"Sisi Kama wadhibiti tunafanya kazi mbalimbali katika kufanya kaguzi zetu ambazo tunakagua miundombinu ya Tanesko, ufanyaji kazi wa Tanesko,kwa hiyo katika kipindi Cha mwaka mmoja hivi tulikuwa tulifanya kaguzi mbalimbali na tumekutana na baadhi ya changamoto ambazo tumeona zinatokana na uelewa kwamba mdhibiti ni nani na anafanya kazi gani"Alisema Lorivi.
Katika hatua nyingine amesema kuwa wanawaelimisha ili wajue mdhibiti amepewa jukumu hilo kwa mujibu wa Sheria na wanawajibika kwa mdhibiti katika kutoa taarifa kwa kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya ufanyaji wa kazi wa maswala mazima ya umeme.
Hata hivyo amesema kuwa changamoto zilizopo ni utoaji mbaya wa huduma kwa wateja hivyo elimu hiyo itasadia kuondoa changamoto hizo na kuboresha huduma huduma.
Mhandisi Evarist Simon ni mkaguzi mkuu wa umeme wa EWURA nchini amesema semina hiyo itasaidia kujadili na kutatua changamoto na mapungufu yaliyopo katika utolewaji wa huduma za nishati kwa wananchi na kuboresha zaidi huduma hiyo.
Mhandisi Evarist Simon ni mkaguzi mkuu wa umeme wa EWURA nchini amesema semina hiyo itasaidia kujadili na kutatua changamoto na mapungufu yaliyopo katika utolewaji wa huduma za nishati kwa wananchi na kuboresha zaidi huduma hiyo.
Amesema kuwa katika Semina hiyo wamelenga maeneo matatu kwenye upande wa ufundi na upande wa kanuni ambazo Ewura wanazitunga kutoka kwenye Sheria mama ya mwaka 2018 ya umeme .
Awali akizungumza kuhusiana na mapungufu yaliyopo kwenye utolewaji wa huduma za TANESCO kaimu meneja Kanda ya Kaskazini mhandisi Charles Urio anaeleza zaidi huku akitoa rai kwa wananchi kuzingatia sheria katika matumizi ya huduma.
0 Comments