Header Ads Widget

MAPATO YAONGEZEKA UWANJA WA KILIMANJARO INTERNATIONAL AIRPORT (KIA)

 


Katika mwaka wa fedha 2020_2021 dunia ilikumbwa na ugonjwa wa korona ambao umesababisha Uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro Airport   kurudi nyuma na kufanya sekta nyingi nchini kuyumba ikiwemo secta ya anga.



Katika kipindi hicho mashirika mengi ya ndege yalilazimika kusimamisha shughuli zake Kama njia mojawapo ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo .



Akitoa taarifa mbele ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kaimu mkurugenzi wa uwanja wa  ndege wa kimataifa Kia Christene Mwakatobe amesema kuwa katika kipindi hicho mapato yalipungua na kusababisha uogozi kubana mapato na matumizi na kusimamisha kwa muda shughuli za maendeleo.



Aidha amesema kuwa mkakati huo umeweza umeweza kufanya shughuli za kiuendeshaji bila kuomba ruzuku yeyote kutoka Serikali.



"Nieleze tu kwamba sisi Kama kdco hatupati mapato yeyote kutoka Serikali ,mapato yanayopatikana hapa ndio yanayotumika katika kuendeleza Uwanja ,lakini vilevile Kuwekeza katika miradi Ya maendeleo ,kwa hiyo tulipopata janga la korona iliathiri sana secta ya utalii na mashirika Ya ndege yalikuwa hayatui hapa katika kipindi flani mpaka ilipotimia tarehe 1julai mwaka Jana ndio tulipoanza kazi tena lakini tuliweza kujipanga upya na kuweka mikakati upya Alisema



Amesema kuwa katika kipindi Cha miaka mitatu iliyopita kampuni imepata mafanikio mbalimbali Kama kupata mafanikio ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kupata mashirika mapya ,kununua mashine 6 za kisasa za kufanyia ukaguzi wa mizigo na kufunga mfumo Mpya CCTV sisystem pamoja na kupata maafisa 7 waliofuzu na kutunukiwa vyeti vya ngazi ya juu ya uendeshaji wa viwanja vya vya kimataifa(international airport professional).



Amesema kuwa mbali na mafanikio Kuna changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na uchakavu wa maghala ya kuhifadhia mizigo,uchakavu wa magari ya zimamoto,pamoja na mgogoro wa ardhi ambao umekuwepo tangu miaka ya nyuma na Serikali inafanya mpango wa kulitatua ambayo hiyo imesababisha ucheleweshwaji wa kuendeleza Uwanja huo.



Hata hivyo amesema kuwa kadco imejiwekea mpango mkakati wa maendeleo wa kuhakikisha kuwa kiwanja hicho kinakuwa na kusongonga mbele ambayo ni pamoja na kukitangaza kiwanja ,kuongeza mapato yanayotokana na kitua kwa ndege na shughuli zingine za zinazofanyika uwanjani,kushirikiana na viongozi kuhakikisha kuwa migogoro ya ardhi inatatuliwa kwani matarajio no kwamba mgogoro huo utaisha kabla ya mwaka 2023.




Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai amemshukuru mkurugenzi huyo kwa kumualika yeye na kamati ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutembele na kujionea kazi zinazofanywa katika Uwanja huo .


Amesema kuwa kutokana na mifumo iliyowekwa katika Uwanja huo inaonesha ni jinsi gani abiria anavyokuwa salama .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI