NA THABIT MADAI,ZANZIBAR
KUELEKEA Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Wizara ya Madini na Taasisi zake wameshiriki katika Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara,yanayoendelea katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kamshina wa Madini Dkt Abdurhman Mwanga amesema ushiriki wao katika Maonyesho hayo ni kuonyesha kwa namna gani kuna fursa mbalimbali za Uwekezaji katika sekta ya Madini.
"Katika Maonesho hayo tumekuja na Madini mbalimbali kwa lengo la kundela kutoa elimu kwa Wananchi waliopo Visiwani Zanzibar kuwa kuna fursa ndani ya Sekta ya Madini," alisema Dkt Mwanga.
Hata hivyo alibainisha kuwa Wamekuja katika Maonesho hayo kuonesha Mazao mbalimbali yanayopatikana kupitia Sekta ya Madini na kwa namna gani walivyofanikiwa.
Kwa Upande wake Kaimu Katibu Mkuu Mtendaji wa TIETI alisema Kuwa lngo la kushiriki katika Maonesho hayo ni pamoja na kutoa Elimu juu ya Shughuli zinazofanywa na TeiTi katika Sekta nzima ya Madini.
"Kikubwa tunachofanya ni kutoa Elimu juu ya Majukumu ya TeiTi pamoja na Wananchi waweze kutuma Taarifa zao kwetu katika kuboresha hii sekta ya Madini," alisema
Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini zinazoshiriki ni pamoja na Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania(GST), Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) pamoja na Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania (TAWOMA)
Maonesho hayo yenye kaulimbiu inayosema, Tumia Bidhaa za Tanzania, jenga Tanzania yalianza tarehe 03 Desemba, 2021 yanatarajiwa kumalizika tarehe 09 Desemba, 2021.
0 Comments