Header Ads Widget

JAMII YA KIFUGAJI YATAKIWA KUTUNZA MISITU.

 



 

Jamii za kifugaji zimetakiwa kuwekeza katika mazingira kwa kupanda miti kwa ustawi wa viumbe hai ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na uhakika wa chakula na nyanda za malisho.........NA NAMNYAK KIVUYO, MANYARA.



 

Akizungumza na wananchi kutoka  vijiji 13 wakiwemo madiwani na wenyeviti wa vijiji kutoka wilaya ya Ngorongoro na Babati Vijijini wakati wakipewa   elimu juu ya utunzaji wa mazingira na uendelezaji wa misitu jamii Meneja wa Mradi wa uhifadhi na uendelezaji wa ikolojia ya Serengeti kutoka Shirika la Kimataifa la Uhifadhi la  Frankfurt  Zoological  Society(FZS), Masegeri Tumbuya alisema kuwa ipo haja kwa wananchi kutunza mazingira ya misitu kwa maslahi ya sasa na vizazi vijavyo.

 

Tumbuya alisema kuwa ipo haja kwa jamii kupunguza shughuli za kibinadamu katika maendeo ya misitu na vyanzo vya maji ili kuwa na uhakika wa ustawi wa viumbe hai.

 

“Katika hali ya kawaida tumekuwa na changamoto mbalimbali mojawapo ikiwa ni shughuli za kibinadamu za kawaida zinaathiri mazingira tukaona ni vizuri wakati tunajiendeleza kimaisha tutoe elimu ya utunzaji mazingira,”amesema

 



“Ukienda Loliondo mji unakua kwa kasi kubwa,na kwa sababu ya kukua kwa miji yetu inapelekea matumizi ya rasilimali za misitu yanaongezeka yakiongezeka bila mpangilio na kusimamiwa vizuri madhara yakakuwa  makubwa,”Alifafanua Tumbuya.

 


Kwa upande wake Mhifadhi misitu kutoka wakala wa misitu Tanzania(TFS),wilaya ya Babati, Paulina Hussein alisema misitu ya katika  jamii inatoa fursa nyingi ikiwemo za kiafya na uchumi.

 

“Misitu  ikisimamiwa vizuri hatutapata madhara kwa  sababu jamii imeshatambua umuhimu wa misitu na sisi tutaendelea kutoa elimu kwa jamii kwani wananchi wakishatambua na kuelewa umuhimu wa misitu watatunza na kuhifadhi misitu ikiwemo kupanda miti,”

 

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Ayasanda, Ally Shabani aliitaka  jamii kuhakikisha kila mmoja anakuwa balozi wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya manufaa yao wenyewe ikiwemo upatikanaji wa maji.

 


“Kila mwananchi ni balozi wa kulinda au kuhifadhi mazingira na lazima tuwe waadilifu na niwaombe tukiondoka tukafundishe na wenzetu ili tuweze kushirikiana kuhifadhi mazingira,”Alisema.



Mmoja wa wananchi hao kutoka Tarafa ya Loliondo Laloposi Meishook alisema elimu hiyo itawasaidia sana kwani awali hawakuwa watutunza mazingira ikiwemo misitu hivyo watakuwa mabalozi wa utunzaji wa mazingira.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI