Header Ads Widget

MKUU WA USALAMA BARABARANI MKOANI RUVUMA AWATAKA MADEREVA WA MALORI KUJALI USALAMA WA BARABARANI.

 






Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani (RTO)Mkoa wa Ruvuma Salum Morimori amewataka madereva wa malori kuheshimu alama za barabarani ili kudhibiti ajali zinazoweza kuzuilika........Na Amon Mtega,  Songea.


Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na madereva wa magari ya malori ambao wanabeba makaa ya mawe kutoka Kijiji cha  Amani makolo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma na kuyapeleka mikoa mbambalimbali ya nchi na nje ya nchi bapo kikao hicho kilifanyika kwenye sehemu ya kuegeshea magari kijijini hapo.


Amesema kuwa dereva anayejielewa ni yule anayesema na lugha za barabara ambazo zinasema usiende mwendo mkali, usiipite gari iliyopo mbele yako sehemu isiyostahili, mteremko mkali, eneo la maegesho ya magari kwaajiri ya kupumzika na si vinginevyo.


Amesema kuwa uendeshaji wa magari makubwa unahitajika umakini mkubwa  ili kuweza  kujihami mwenyewe na umuhami na mwenzio ambaye pia Ni mtumiaji wa barabara hivyo ni vyema kutii sheria bila shuruti za usalama barabarani.


"Tunamuona dereva ni mtu muhimu sana kwenye maisha ya kila mtu isipokuwa kazi hii imeingiliwa, imechafuliwa na baadhi yetu kwa matumizi mabaya , tumeshuhudia matukio mbali mbali kupitia barabara ni vyema mkatambua kuwa mstakabali wa maisha yenu ndio mstakabali wa maisha ya wengine" amesema Morimori.



Aidha amewataka kushirikiana na jeshi la Polisi kutoa taarifa pindi wanapoona vyombo vyao vinahitilafu au dereva mwenzao anendesha huku amelewa badala ya kuwaona Polisi ni maadui wajenge urafiki ili waweze kupunguza hajari zinazoweza kudhuirika.


Kwa upande wake Inspekta msaidizi wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Ruvuma Lilanga Chodas amesema kuwa madereva wengi hataki kufuata sheria za usalama barabarani bila kujari kuwa serikali imewekeza kwenye miundombinu kwa fedha nyingi lakini pia kujari maisha ya wengine watumiaji wa barabara.


Nao madereva wa malori wameshukuru ofisi ya RTO Mkoa wa Ruvuma kwa nmana Askari wa kikosi cha usalama barabarani kinavyofanya kazi tofauti na maeneo mengine ya mikoa kama Chimala, Senkenke, Muleba, Bai na Kifanya wamekuwa wakiwasomea tochi za uongo na kuwatajia spidi zisizo alali kwani wengi wao magari yao yamefungwa GPS.


Wameomba serikali kuangali vituo hivyo vilivyotajwa kwani madereva wengi wamekuwa wakionewa kwa kupigwa faini zisizo halali na mala nyingine wanatishiwa kupelekwa mahakamani.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI