Header Ads Widget

ACT YAIBOMOA NGOME YA CUF TUNDURU

Viongozi wote wa Chama Cha Wananchi (CUF) Kata ya Tinginya Jimbo la Tunduru Kaskazini mkoani Ruvuma wamejiengua kwenye chama hicho na kujiunga na ACT Wazalendo.


Tukio hili limetokea jana Desemba 9,2021  wakati Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ndugu Ado Shaibu alitembelea kata hiyo kushukuru wananchi waliomuunga mkono na kumpigia kura za ubunge katika Uchaguzi Mkuu 2020.




"Nilipita hapa majuzi kuwashukuru Wanachama wa ACT Wazalendo na wadau wengine walionisaidia mimi na chama kwa hali na mali kwenye Uchaguzi Mkuu 2020.


Jana nilipata wito wa viongozi wa CUF wa Kata ya Tinginya walionitaka nirudi kwa ajili ya mazungumzo.


"Walisema wameguswa na kitendo changu cha kupita kushukuru licha ya kudhulumiwa kwenye Uchaguzi. Viongozi hawa wa Kata ya Tinginya kama ilivyokuwa kwa viongozi na wanachama wengi wa CUF Tunduru, kinyume na maelekezo ya chama chao, waliniunga mkono nilipogombea Ubunge katika Jimbo la Tunduru Kaskazini. Walitanguliza mbele maslahi ya Tunduru na mageuzi kuliko ya chama chao. 


"Jana waliponiita walisema bayana kuwa kitendo changu cha kuja kushukuru kimewatia moyo sana na wameona ACT Wazalendo ni jahazi sahihi hivyo wameona bora wajiunge nalo. "Alisema Ado


Katika tukio hilo, Ado alikabidhi kadi za ACT takribani kwa uongozi wote wa CUF Kata ya Tinginya na vijiji vyake vya Tinginya, Tanga na Namatanda wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kata hiyo, Mshamu Shaibu Baniani, Katibu Salumu Mussa Bomba na aliyekuwa Mgombea udiwani wa kata hiyo, Mohamed Issa Ndayani.


Kata ya Tinginya inafahamika kwa kuwa na mwamko mkubwa wa siasa za mageuzi Wilayani Tunduru.


Ado anaendelea na ziara ya kushukuru wananchi wa jimbo hilo licha kuwa hakushinda katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI