Header Ads Widget

SMZ YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA ITALY KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA KIMAENDELEO

 


JUMLA ya Wabunifu 4 Wazawa wa Mavazi ya Kitamaduni Wameshiriki katika Tamasha la Maonesho ya Mavazi ya Mbalimbali ya Kitamaduni liloandaliwa na Ubalozi wa Italy kwa kushirikiana na Uongozi wa  hotel ya Park Hayyat.


Tamasha hilo ni Muendelezo wa Kusherekea Wiki ya Utamaduni wa Chakula na Mavazi ya Asili ya Kitaliano ambapo limefanyika katika Hotel ya Park Hayyat Mji Mkongwe Mjini Unguja na Kuhudhuriwa na Wanamitindo maarufu kutoka ndani na Nje ya Tanzania pamoja na Viongozi wa Serikali na Taasisi mbalimbali Binafsi.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kukamilika kwa Tamasha hilo la Maonesho ya Mavazi, Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwezeshaji Zanzibar  Mudrik Ramadhani Soraga Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuhakikisha wanadumisha Ushirikiano baina yake na Serikali ya Italy Katika Nyanja ya Mbalimbali za Kimaendeleo.


Amesema Mashirikiano hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kufungua Fursa za Kiuchumi kwa Wageni wengi wa Italy kuja kuwekeza Zanzibar.


“Kama tunavyofahamu kuwa Hotel nyingi za Zanzibar zinamilikiwa na Wawekezaji kutoka Italy hivyo kama Serikali tutaongeza Mashirikiano ili kukaribisha zaidi wawekezaji kutoka Italy kuja Zanzibar,” alisema.


Aliongeza kuwa Tamasha hilo ni matunda ya Mashirikiano baina ya Tanzania na Serikali ya Watu wa Italy.


Hata Hivyo Waziri Soraga alitumia fursa hiyo kuwakaribisha Wageni mbalimbali kuja kuwekeza katika Sekta ya Utamaduni.


“Leo Usiku Wenzetu wa Italy wameandaa maonesho haya ya Mavazi na kuunga Mkono Utamaduni wetu, hivyo niwakaribishe Mataifa mengine kuja kuwekeza katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Utamaduni,” alieleza Waziri Soraga.


Nae Balozi wa Italy Nchini Tanzania Marco Lombard amesema kupitia Matamasha kama hayo ya Mavazi yatafungua fursa mbalimbali za Uwekezaji katika Nyanja tofauti tofauti.


Aidha alisema kuwa Italy itaendelea kuunga Mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaletea Maendeleo Wananchi wake.


“Tumekuwa kwa karibu tukifanya kazi na ZIPA katika Masuala mbalimbali ya Uwekezaji na Maendeleo, Italy inaunga Mkono juhudi za Serikali katika Manedeleo ya Nchi,”alisemaa.


Kwa upande wake Mwanamitindo Mpya Faida Kanda alisema kuwa Amefarajika kuwa Miongoni mwa Washiriki wa Maonesho hayo ya Mavazi Visiwani Zanzibar.


“Nataka Niwashauri Wananchi mbalimbali wasiwe nyuma wajitokeze kwa Wingi kuja kuungalia maonesho kama haya ya Mitindo ya Mavazi na kudumisha utamaduni wa Kiafrika,” alieleza.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI