Header Ads Widget

WAZIRI AWESO AZINDUA MRADI WA MAJO MLANDIZI MBOGA

 


Na Scolastica Msewa,MDTV  Chalinze 

WAZIRI wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani Mkoani Tanga Jumaa Aweso amefungua mradi wa maji wa Mlandizi Mboga ambao umekamilika kwa asilimia 98 wenye thamani ya shilingi bilioni 18 huko Chalinze mkoani Pwani.



Aweso amefungua Mradi huo wakati alipofika kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi huo na mara baada ya kumaliza ziara yake kwenye mradi wa maji Mlandizi-Chalinze- Mboga akafungua Mradi huo akimaanisha kuruhusu wananchi kuendelea kupatiwa maji.


Waziri wa Maji amekagua na kuridhika kuruhusu maji yaanze kutumiwa na wananchi katika maeneo ya Chalinze ambapo miundombinu imekamilika. 


Aidha Mheshimiwa Aweso ameagiza uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha wanawainganishia wateja wa maji huduma ndani ya siku 14 isizidi hapo vinginevyo wakizingua atawazingua.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI