Header Ads Widget

MADIWANI KIBAHA MJINI WALALAMIKA KUPANGIWA MATUMIZI YA FEDHA

 


BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kibaha mkoani Pwani wamelalamikia kupangiwa matumizi ya fedha wanazoomba na kutumika kwenye miradi ambayo hawajaiombea fedha kwa madai ni maelekezo toka juu.


Akiongea kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Kibaha mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mussa Ndomba amesema kuwa hali hiyo inasababisha miradi kukwama ambapo madarasa 14 yameshindwa kujengwa na mengine kukarabatiwa.


Ndomba amesema kuwa maelekezo hayo hupewa wataalamu wa Halmashauri kuwa fedha fulani zipelekwe sehemu fulani licha ya baraza la madiwani kupanga bajeti kwenda kwenye maeneo yenye uhitaji.


Amesema wataandika barua kwa Rais kulalamikia hali hiyo kwani wanaofanya hivyo wanakwamisha bajeti za Halmashauri hiyo kwa sehemu zenye changamoto kutopatiwa ufumbuzi kupitia miradi.


Diwani wa kata ya Visiga Kambi Legeza ambaye aliibua hoja hiyo amesema kutokana na hali hiyo ni mbaya kwa madarasa hayo kukosekana wanafunzi wengi wanasoma kwenye mazingira magumu. 


Legeza amesema kuwa wasingependa kuingiliwa kwani wako kisheria hivyo wasingependa kuona kile wanachokipitisha kinabadilishwa kwa maslahi ya watu wachache.


Naye mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa hoja hiyo ni nzito kwani suala hilo linasababisha  hangamoto kwani tayari tathmini inakuwa imefanyika.

Munde amesema kuwa wataendelea kukumbusha kuzingatiwa kwa maazimio ya baraza na anaamini hilo litazingatiwa kwa bajeti zijazo.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI