Header Ads Widget

UBUNGE CCM VUNJO AIBU TUPU, GENGE LA UHARIFU LADAIWA KUKUTWA NA SIRAHA ZA KIGAIDI

 


Na Matukio Daima Media ,Vunjo

UCHAGUZI wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mpinduzi (CCM) jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro umemalizika huku ukiacha makovu mengi kwa wakazi wa maeneo hayo na vitongoji vyake.

Uchaguzi huo uliokuwa na jumla ya wagombea ubunge sita umeacha majeraha ya kutisha huku mmoja wa wagombea hao kudaiwa kuratibu genge la mauaji lililosababisha baadhi ya raia kujeruhiwa na wengine kunusulika kuuawa.

Baadhi ya vijana wamekamatwa wanadaiwa kujihusisha na genge hilo likiwa na vifaa hatari kama vile kamba za kunyongea watu, mabomu, risasi, mapanga na vifaa vingine vinavyotumika kufanya ugaidi.

Mmoja wa makada wa CCM kutoka Kata ya Makuyuni ambaye ameomba jina lake lisitajwe kwa sababu za kiusalama amesema kuwa matukio hayo yameacha baadhi ya raia wakijeruhiwa na wengine kunusulika kuuawa.

Alisema usiku wa kuamkia siku ya upigaji kura za maoni, yaani Agosti 4,2025 liliibuka kundi la waharifu ambalo liliwajeruhi baadhi ya vijana waliokuwa wanafuatilia nyendo zao

Kada huyo alimtaja mmoja wa majeruhi kwa jina moja la Safina ambaye tayari amefungua jalada la kesi katika kituo cha Polisi Himo kwa hatua zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa baadhi ya watu wanadaiwa kujihusisha na genge hilo na kwamba hatua za kuwafikisha mahakamani zinaendelea ikiwa ni pamoja na kufanyia uchunguzi ili kubaini ni akina nani wako nyuma ya mtandao huo.


RPC Maigwa amesema kuwa genge hilo limekutwa na vitu mabalimbali vya kihalifu na kwamba uchunguzi wa kina utakapo kamilika taarifa kamili itatolewa, hivyo amewataka wananchi kuwa na subira wakati uchunguzi ukiendelea.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi alipoulizwa juu ya suala hilo alisema atafutwe aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni katibu wa chama hicho ngazi ya mkoa.


Aidha taarifa kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro zinaeleza kuwa gege hilo liliratibiwa kwa karibu na mmoja ya wagombea kwa lengo la kuvuruga uchaguzi baada ya kubaini upepo mbaya wa kisiasa ukivuma upande wake.


Taarifa hizo zinasema mmoja wa vijana wanaoshikiliwa na jeshi la polisi wakihusishwa na genge hilo ni mmoja wa wanafamilia wa mke wa mgombea ubunge jimbo la Vunjo ambaye jina lake linahifadhiwa hadi tutakapompata ili azungumzie suala hilo.


Matokeo ya kura za maoni katika jimbo la Vunjo mwaka huu ni kama ifuatavyo, Enock Koola aliibuka mshindi kwa kupata kura (1999), Dkt Charles Kimei (861), Yuvenal Shirima (659), Didas Lyamuya (329),Prosper Tesha (177) na Delfina Kessy aliambulia kura (29).



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI