Na, Titus Mwombeki-MTDTV Kagera.
Wazazi pamoja na walezi mkoani Kagera wameshauliwa kuwapeleka watoto wao ambao wameishafikisha umri wa miaka 18 katika vituo vya afya waweze kupatiwa chanjo ya UVIKO 19 ili kuwakinga watoto hao dhidi ya ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa bodi ya shule ya Kaizirege na Kemeboss Hajji Abubakari Kagasheki katika mahafali ya darasa la saba na kidato cha nne yaliyofanyika katika shule hiyo iliyoko kata ya Ijuganyondo halmashauri ya Bukoba mkoani kagera.
“Shule zetu zinawanafunzi wengi ambao wamefikisha umri wa miaka 18 wamekizi vigezo vya kupatiwa chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 hivyo niwajibu wetu sisi kama wazazi au walezi kuhakikisha tunawatunza watoto wetu wanakuwa salama kwa kuwapeleka au kuwashauri watoto wetu waende katika vituo vya afya wakapate chanjo ya ugonjwa huu kwani bado upo”
Mwenyekiti Kagasheki ameongeza kuwa wazazi waache tabia ya kusikiliza maneno ya watu ambao wanasema kuwa chanjo ya UVIKO 19 inamadhara kitu ambacho sio kweli kwani yeye binafsi pamoja na familia yake walichanja na mpaka sasa wako vizuri kiafya na hawajaona madhara yoyote ya chanjo hiyo.
Kwaupande wa Askofu mstaafu wa Anglikan mkoani kagera Jacton Rugumila ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo amesema kuwa watoto ndio taifa la kesho kwahiyo wanatakiwa kujengwa katika misingi mizuri ili kujenga taifa lenye ustawi.
“ Watoto hawa ndio taifa la kesho tukijengwa katika misingi mizuri na imara tutaweza kujenga taifa imara, taifa lenye ustawi, taifa lenywe watu wanaoaminika lakini pia taifa la watu walioandaliwa vizuri, shule ya Kaizilege na Kemiboss imekuwa ikiwajenga watoto hawa katika misingi hiyo ndio maana hata ufaulu wake umekuwa ukipanda kila mwaka tangu shule hii ianzishwe” amesema askofu Rugumila.
Naye meneja wa shule hiyo Eulogius Katiti akisoma taarifa ya shule hiyo mbele ya mgeni rasmi amesema kuwa shule hiyo imekuwa kufanya vizuri kitaaluma kila mwaka na kujipatia tuzo mbalimbali na hii nikutokana na mshikamano na kujituma kwa wafanyakazi, wanafunzi pamoja na miundombinu ya shule hiyo kuwa nzuri.
“Nachukua nafasi hii kuwashukuru wageni wote ambao mmeweza kujumuhika nasi, tumeweza kushuhudia shule yetu ikieendelea kukua kitaaluma na kimaadili na haya yote ni kutokana na mshikamano tulionao wafanyakazi washule hii kwa kushirikiana na viongozi wakiroho lakini pia miundombinu bora na yakisasa inayopelekea wanafunzi wetu kusoma vizuri bila bughuza yoyote, kutokana na ufaulu huo shule yetu imeweza kujinyakulia tuzo nyingi za kitaaluma nchini ikiwemo tuzo ya rais ya utunzaji wa mazingira na upandaji miti”
Ameongeza kuwa katika kuongeza ushindano wa kitaaluma mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Yusto Kaizirege Ntagalinda kwa kushirikiana na mama mkurugenzi Bi. Elizabeth Kaizilege wameanzisha tuzo maalumu kwa wanafunzi wao ihitwayo ‘THE KAIZIREGE AND KEMIBOSS ACADEMIC EXCELLENCE AWARD’ .
“Tuzo hii itawahusu wanafunzi watakaoweza kuingia kwenye orodha ya wanafunzi 10 bora kitaifa na wale watakaoweza kuongoza kimasomo nafasi ya kwanza hadi nafasi ya ya 5 kitaifa, zawadi au tuzo hii itakuwa ni kusoma bure kwa miaka miwili katika shule za Kaizirege na Kemiboss” amesema Katiti.
Akisoma risala iliyoandaliwa na kidato cha nne ambaye ni mhitimu katika shule hiyo Eren Eulogius Katiti ameushukuru uongozi washele hiyo na kuahidi kuwa kutokana na maarifa bora waliyoyapata katika shule hiyo watayatumia vyema katika kuliletea taifa faida.
“Tunaushukuru uongozi wa Kaizirege na Kemiboss na tukielekea katika mitihani yetu ya kumaliza kitado cha nne itakayoanza tarehe 15 mwezi Novemba mwaka huu tunaamini sote tutafaulu mitihani yetu, tunaahidi kuwa elimu tuliyo hipata katika shule hii tutaitumia vyema ili ikalinufaishe taifa letu”
0 Comments