Header Ads Widget

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kujisajili kwenye mradi mkubwa unaokutanisha wafanyabiashara zaidi ya 250 ambao unasimamiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF). mwandishi wa matukio daima Fatma Ally anaripoti kutokea Dar es Salaam

Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Francis Nanai wakati alipokua akizindua mradi huo wenye lengo la kukuza, kuzilea na kuziwezesha brandi changa za kitanzania zipatazo 100.

"Huu tunaona ni mwanzo mzuri, tunaomba wafanyabiashara wa kitanzania wajitokeze kwa wingi kujisajili katika mradi huu mkubwa ili brandi zao ziweze kulelewa na kuendelezwa, pamoja na mambo mengine waweze kutangaza biashara zao kimataifa na kuwa na majina makubwa"amesema Nanai.

Alisema kuwa,kuwepo kwa mradi huo kutaongeza walipa kodi wengi nchini na kuongeza uchumi wa Tanzania kukua pamoja na kuonesha uwezo walionao watanzania katika masuala ya biashara, ambapo utafanya kazi kwa miezi 48 kuanzia sasa ulipozinduliwa Hadi kufikia January 2025 utakua umekamilika.

Aliongeza kuwa, pamoja na mambo mengine watanzania wataweza kupata fursa za kutangaza biashara zao kuanzia Afrika Mashariki hadi duniani kote ambapo hadi kukamilika kwa mradi huo kutaweza kutengeneza ajira rasmi 38,250 na zisizorasmi 56,250.

"Miongoni mwa vigezo ambayo vitamuwezesha mfanyabiashara kuweza kushiriki katika mradi huo lazima awe na biashara ambayo ina umiliki wa kitanzania, awe na leseni, analipa kodi,awe na mtaji usiopungua shill mill 250 pamoja kukaguliwa kwa miaka mitatu mfululizo"amesema Nanai.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha wafanyabiashara  wanawake Tanzania (TWCC) Mwajuma Hamza, amesema kuwepo kwa mradi huo kutaongeza wigo wa biashara kwa wafanyabiashara wakiwemo wanawake  kuweza kufanya biashara zao kimataifa zaidi 

Aidha, alisema kuwa mradi huo utawajengea uwezo na kuwaenua wanawake kwani hiyo ni fursa nzuri ya kuweza kutangaza na kuuza biashara zao kimataifa pamoja na kukuza brandi zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI