Header Ads Widget

UNICEF YATOA MAFUNZO KWA WANASHERIA

CHUO cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya watoto (UNICEF) wametoa mafunzo kwa wadau wa sheria wanaoshughulika na masuala ya haki za mtoto juu ya uendeshaji wa mashauri ya mtoto mbele ya mahakama na namna gani mashauri hayo yanatakiwa kuendeshwa pale mtoto akiwa amekizana na sheria. mwandishi wa matukio daima Hamida Ramadhani anaripoti kutokea Dodoma

Lakini pia ni mafunzo hayo yametolewa kwa wadau wanaoendesha mashauri mahakamani kuanzia majaji na mahakimu,waendesha mashitaka wa serikali na maafisa ustawi wa jamii kwani kuna wakati mwingine mtoto anaweza kuwa muathirika au muhanga au mtuhumiwa.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada ya kufungua mafunzo hayo ya siku tano Dkt Poul Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama ya Lushoto amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwaeleza sheria inasemaje kwani mtoto kutokana na umri wake na uwezo wa kutokuwa na akili ya utu uzima anavyostahili kutendewa na hata sheria imeelekeza afanyiwe tofauti na watu wazima .

" Mahakama inaposhulikia mashauri ya mtoto manake mahakama iendeshwe kwa mfumo wa faragha kesi haikai katika mazingira ya hali ya kawaida na mtoto kuna aina ya maswali ya kumuuliza ,"amesema jaji Kihwelo .

" Tunawapa mafunzo kundi la watu 40 ambao na wao watakwenda kutoa elimu hiyo kwa watu wengine na niseme tu wazi mafunzo kama haya tuliwahi kuyafanya mwaka 2014 kwani wengi  wamestaafu na wengine mahakimu wamekuwa majaji hivyo tumeona ni vyema tufundishe kundi jingine na sasa tumewaleta waendesha mashitaka wa serikali ili kujadili changamoto wanazokumbana nazo kwenye uendeshaji wa mashauri ya mtoto anapokuwa mahakamani," amesema 

Naye Dkt Aneth Mzava kutoka chuo cha Uongozi wa mahakama ya Rushoto mhadhiri na Mratibu wa Mradi wa Haki za mtoto unaoratibiwa na UNICEF na Chuo hicho cha Uongozi wa Mahakama ya Lushoto amesema sababu ya kutoa mafunzo hayo ni kuona namna bora ya kuendesha mashauri ya watoto na namna bora ya kutoa haki pale mtoto anapokizana na sheria.

Amesema Kama tunavyofahamu sheria ya mtoto ya mwaka 2009 hivi karibuni mwaka 2019 inaonyesha ni namna gani  mtoto anapokuwa amekizana na sheria ama shauri lake  linatakuwa kusikilizwa  mahakamani watambue mashauri hayo hayaendeshwi kams mashauri ya watu wazima.

Kwa upande wake  Hakimu mkazi mwandamizi Rhoda Ngimilanga kitengo cha watoto mahakama kuu masijala kuu amesema wapo kwenye mafunzo hayo kwani eneo la mtoto limekuwa na changamoto .

" Ni kweli sheria ya mtoto inatumika ile sheria ya mwaka 2009 sura ya 13 sheria hiyo inatumika kuanzia tukio linapo tokea mtoto anapokinzana na sheria  namna gani anaweza kushughulikiwa," amesema 

Kwa upande wa madai Jaji Ngimilanga amesema mashauri yanasikilizwa yanahusu ulinzi wa mtoto matunzo ya watoto na haki mbali za watoto mashauri yanasikilizwa pia.

Akielezea sheria ya mtoto kwa upande wa kutoa adhabu amesema mtoto hafungwi mtoto mpaka anakwenda kuwekwa kwenye kizuizi ni hatua ya mwisho na hivyo mtoto anawekwa katika maadili tu lengo ni kumbadilisha ili aweze kuwa raia mwema kwani anauwezo wa kubadilika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI