Imeeelezwa kuwa mabadiliko ya tabia ya Nchi yanapotokea wanaoathirika zaidi ni watoto na akina mama ambao wao ndio wamekuwa wazalishaji wakubwa ukilinganisha na akina baba. mwandishi wa matukio daima Rehema Abraham anaripoti kutokea Kilimanjaro
Pia wafugaji nao wamekuwa wakiathirika kwani mifugo imekuwa ikifa kwa kukosa maji na kusababisha umakini kwa wafugaji hao .
Hayo yamesemwa na Elias Mtinda meneja kilimo na chakula shirika la action aids internation wakati alipokuwa akizungumza mkoani Kilimanjaro kwenye hafla ya kutoa elimu ya mdhara ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Aidha amesema kuwa wanaosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi ni nchi zilizoendelea Kama marekaani china ambayo kwa kiwango kikubwa wamekuwa wakizalisha hewa ya ukaa ambayo imesababisha mabadiliko ya tabia ya nchi inaayoathiri nchi zinazoendelea Kama Tanzania.
"Kwa sababu nchi zilizoendelea ndizo zinazosababisha changamoto hii tumekuwa tukiita kwamba nchi hizo ziweze kutoa fedha kwa ajili ya kusaidia nchi zinazoendelea ili ziweze kuhimili mabadiliko ya tabia ya nchi na wakulima na wafugaji waweze kusaidiwa na wahimili mabadiliko ya tabia ya nchi"Alisema.
Katika hatua nyingine amesema kuwa nchini mbalimbali zimesaini mikataba ya kimataifa juu Ya namna ya kupunguza utoaji wa hewa ukaa ambayo inaleta madhara kwa wazalishaji na wakulima wadogo ambapo mpaka Sasa utoaji wa fedha hizo umekuwa changamoto.
Amesema kuwa ni vyema halmashauri ikatenga fedha kwa ajili ya kusaidia vikundi mbalimbali viveze kutunza mazingira.
Akiwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Naibu msatahiki mea wa manispaa ya Moshi Stewart Nkindi Amesema kampeni hiyo itawasaidia wananchi kutambua namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuangalia njia za kuweza kukabiliana na hayo.
"Mabadiliko hayo yaliyosababiahwa na matumizi mabaya ya mazingira Kama ukataji wa miti hovyo ,ukuaji wa viwanda ambayo imekuwa ikitoa hewa isiyofaa inayoharibu lile tabaka kule juu ya angani ambalo linalinda jua lisiweze kuwaka "Alisema.
Amesema kuwa mkoa wa Kilimanjaro limekuwa eneo lililoathirika kwa kiasi kikubwa kwani theluji katika mkoa wa Kilimanjaro imekuwa ikiyeyuka na maeneo mengine.
Hata hiyo amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi mazao mengi yamekuwa yakiaathiriwa na magonjwa mbalimbali.
0 Comments