Header Ads Widget

UZINDUZI WA JUKWAA LA HAKI JINAI KUSAIDIA KURATIBU NA KUSHUGHULIKIA KESI ZA WATOTO.

Ukosefu wa uratibu mzuri wa kushunghulikia kesi za watoto hupelekea kesi nyingi za watoto kushindwa kusilikilizwa kwa wakati na kupatiwa haki zao za msingi. mwandishi wa matukio daima Chausiku Said anaripoti kutokea Mwanza

Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel alieleza kuwa kuzinduliwa kwa Jukwaa la Haki Jinai katika Mkoa huo utasaidia  kutimiza matakwa ya sheria na unaendelea kusimamia vizuri huduma za haki jinai kwa makundi yote.

Mhandisi Robert alieleza kuwa pamoja na Mkoa wa Mwanza kusimamia vizuri haki jinai lakini bado kunachangamoto upande wa mahabusu, undeshaji wa kesi, uratibu wa kushugulikia kesi za watoto na mahakama hivyo kuwataka wajumbe wa Jukwaa hilo  kuhakikisha  linatatua changamoto wanazokumbana nazo kwa wadau na jamii kwa ujumla.

"Pamoja na kukosa uratibu mzuri wa kesi za watoto lakini tatizo lingine kubwa linalo waathiri watoto ni ucheleweshwaji wa upelelezi katika kesi nyingi za jinai hii hupelekea kesi nyingi kutofika mwisho" alisema Mhandisi Gabriel.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Mkoa wa Mwanza Rehema Mkinze alisema kuwa kuzinduliwa kwa jukwaa hilo la haki jinai kutatatua mashauri mbalimbali ya wananchi na kuwataka wananchi nao kuhakikisha wanarahisisha kazi ya jukwaa.

Alisema kwenye kesi za watoto ni jukumu la Ustawi wa jamii, Magereza, Mahakama, Polisi Pamoja na Jamii kushiriki kuona haki za watoto walio na kesi zinapatikana.

"Jamii ina jukumu la kutoa ushahidi kwa ajili ya kesi ili kuendelea kupatiwa ufumbuzi na tunatumaini kupatikana kwa jukwaa hili ambalo lina mchanganyiko wa watalaamu kutoka maeneo mbalimbali tunaona haki jinai ikwenda kupatikana" alisema rehema.

Aidha Rehema alieleza kuwa jukwaa hilo litakuwa na wajibu wa kutoa elimu  kwa jamii hususani upande wa kesi za watoto kwa kuwa jamii pia inaonekana kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na sheria ya Mtoto ambayo huelekeza usimamiaji wa kesi za watoto na namna zinavyotakiwa kuendeshwa na hukumu zao zinavyotakiwa kuwa.

Kuzinduliwa rasmi kwa Jukwaa la Haki Jinai mkoani Mwanza kutaharakisha utoaji wa haki mahakamani na kwa mahabusu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI