Header Ads Widget

SIMBA SC YAAMUA MSIMU HUU ,UBAYA UBWELA

Na Leonard johnson.

Nyakati za utukufu zimekaribia na matumaini yanaanza kurejea msimbazi ,hapa hakuna muda wakupumua utafuta jasho ukiwa safarini ,unaambiwa ubaya ubwela ndio utamaduni halisi wa simba sc msimu huu wa mashindano 2025/2026.

kiufupi simba sc ya msimu huu haifananishwi kwa namna ya usajili wanao ufanya ,usajili wa simba sc unazitishia falme nyingi za zoka hapa nchini na nje ya mipaka ya Tanzania ,kila palipo kuwa na mapengo wao wamejaza pamba na kuzalisha jino kamili ,yaani kiufupi kocha msimu huu atarusha jezi atakaye daka ataanza hakuna shida.

Mabibi na mabwana msiseme sikuwambia ,kila ukitazama kikosi cha soka cha simba sc na sajili walizofanya wana simba wanayo nafasi yakusema Tajiri hana deni ,walipo fanya kusafisha kikosi watu hawakumini wanacho kifanya ila kwasasa wanaanza kuwaelewa ,uthubutu mkubwa ndio jadi ya simba sc ,moja kwa moja hadi katika ngome ya Patrice Motsepe Mamelody Sandowns na kumchukua beki kisiki Rushine Deruek Handsome boy wa kizulu ,pengo la Che Malon limezibwa kabla ya msimu kuanza .

Hata hivyo unambiwa hawakuishia hapo kuna miamba imara ilishushwa kimya kimya huku Jonathan Sowah akiwa silaha muhimu ya kuingia nayo vitani msimu huu ,sehemu ya kiungo kuna watu walio hasi kambi ya upinzani wakikana chama nakuamua kuwa muhimili katika msimu huu hapo yupo Yusuph Kagoma,Alasane kante na Jean charles Ahou huku sehemu ya juu washambuliaji wengi tumaini lao likiwa limerejea Elie Mpanzu kibisawala.

Semaji la CAF linatamba lenyewe lina sema msimu huu mtachagua kuzika au kusafirisha gari ya kubeba mzoga atalipia ,vuta picha nyuma mstari wa ulinzi yupo Abdulazack Hamza,Rushine Diruek,kulia Yupo mkongwe wa kazi Shomary Kapombe na kushoto weka hata jiwe shetani havuki mpaka .

mwisho kauli ya Tajiri imesikika leo ikisema hapo bado yaani mpaka wa seme kwani anayeichukia simba sc atapata kisukari ,huku kwa kubembeleza anasema "Tukutane saanne ,kuna tamko muhimu" 



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI