Header Ads Widget

BONAH AKAGUA MRADI WA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA, KIMANGA, BONYOKWA NA KINYEREZI

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Kamol Leo ameanza ziara ya kukagua Mradi wa maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyojengwa kutoka pesa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kupitia kwenye mfuko wa UVIKO 19. mwandishi wa matukio daima Fatma Ally anaripoti kutokea Dar Es Salaam

Akizungumza na waandishi wa habari alipokua katika ziara hiyo, alisema wanaishukuru Serikali chini ya Rais Samia kuweza kutoa kipaumbele katika Sekta ya elimu ambapo ametembelea Shule Sekondari Kisungu,Kinyerezi, Kinyerezi mpya, Bonyokwa pamoja na kimanga.

Alisema lengo la ziara hiyo, ni kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ambapo Jimbo la Segerea lilikua na changamoto ya vyumba vya madarasa hali iliyopelekea baadhi ya wanafunzi kuingia kwa awamu.

"Leo tumeanza ziara kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa hizi ni pesa kutoka kwa Rais, si jambo dogo kuweza kupata pesa zote kwa wakati mmoja na kuweza kujenga madarasa mengi namna hii na haijawahi"amesema Bonnah

Aidha,akielezea mgawanyo wa pesa zilizotumika katika ujenzi huo amesema shule ya Sekondari Kisungu imepewa Jumla ya mill 160 kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa 8, Kinyerezi mpya shill mill 60 kwa vyumba vya madarasa 3, Kinyerezi shill mill 160 kwa vyumba vya darasa 8, Bonyokwa shill mill 240 kwa vyumba vya madarasa 12, pamoja na Kimanga shill mill 80 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 4.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Lea Bernad amesema kata hiyo ilikua na uhaba wa vyumba vya madarasa ambapo katika shule ya Sekondari Kisungu baadhi ya madarasa walifungwa kutokana na kuharibika lakini kupitia mradi huo, anaishukuru Serikali kwa kutoa kipaumbele kwenye elimu kwani wanafunzi walikua wanakaa chini ya mti na wengine wanaingia kwa awamu jambo ambalo lilinapelekea watoto kuweza kujihusisha na vitendo vibaya.

Aidha alisema, licha ya kupatiwa mradi huo lakini bado wanahitaji madarasa kwani wanafunzi ni wengi na uhitaji wa madarasa ni mkubwa, ambapo kupitia mradi huo wamepata Jumla ya shill mill 380 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 21 katika Kata ya Kinyerezi, jambo ambalo limetoa matumaini mapya kwa wanafunzi.

Anord Tenganamba ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kisungu Sekondari amesema kutokana na changamoto ya miinuko iliyopo katika shule yao wanayajenga madarasa hayo kwa ubora wa hali ya juu, ambapo wameanza kwa kulaza mchanga nchi, na baadae kutandika nondo zaidi ya mia moja Ili kueka uimara baadae yasipasuke.

Uongozi wa Shule ya Bonyokwa Sekondari chini Diwani wa Kata hiyo, Tumike Malilo  wamemshukuru Rais Samia kwa kazi nzuri ya kutoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, na kumpongeza Mbunge wa  Jimbo hilo kwa kazi nzuri anayoifanya ya kusimamia na kutekeleza  ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa vitendo.

"Mbunge wetu umekua ukijitoa sana kutatua kero za wananchi unasimamia vyema ilani ya chama Cha Mapinduzi CCM, katika ujenzi mradi upo vizuri tumeshafika hatua ya kufunga linta, pesa zipo katika akaunt ya shule, tunaamini mradi huu utakamilika kwa wakati"amesema Tumike.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI