Picha hii ya mtandaoni ni mfano wa Tsunami iliyopata kutokea
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaungana na nchi nyingine Duniani, kuadhimisha Siku ya Tsunami Duniani ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 5 Novemba kila mwaka.
Lengo kuu la siku ya Tsunami Duniani ni kuhamasisha uelewa juu ya janga la Tsunami ambalo hutokea kwa nadra na kusababisha maafa makubwa kwa maisha ya watu na mali zao. Maadhimisho haya ni ya 6 tangu siku hii ilipoanzishwa mwaka 2015 na Kauli Mbiu ya mwaka huu 2021 inasema, "Kwa umoja wetu pekee tunaweza kutimiza adhma yetu"
0 Comments