Header Ads Widget

SERIKALI YATOA MIL 200 UJENZI WA MADARASA IFIGA KILOLO

Mbunge wa Kilolo Justin Lazaro Nyamoga ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Ifiga iliyopo katika kijiji cha Kihesamgagao  kata ya Ng’uruhe.

Mbunge Nyamoga akiongozana na Diwani wa kata hiyo Pancras Kihanga  pamoja na viongozi wa Halmashauri ya wilaya alichangia jumla ya mifuko 20 ya saruji huku halmashauri ikichangia shilingi Milioni 12 ili kufanikisha ujenzi huo wa madarasa matatu ambapo mpaka sasa madarasa mawili yameshakamilika.

Awali ujenzi wa shule hiyo ulianza kama kituo shikizi baada ya wakazi wa Kitongoji cha Ifigi mifugo kuanzisha ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa ili kuondoa adha ya watoto wao kutembea kwa umbali wa zaidi ya kilomita 10 kwenda na kurudi katika shule ya msingi Kihesa mgagao.

Nyamoga alisema kuwa serikali ya jamhuri ya muungano  wa Tanzania imetoa jumla ya shilingi Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba sita vya madarasa, vyoo vya walimu na wanafunzi pamoja na nyumba moja ya mwalimu ambapo baada ya ujenzi kukamilika shule hiyo itakuwa na jumla ya madarasa tisa.

‘’tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwaunga mkono wakazi wa kitongoji cha ifiga na kihesamgagao katika kutatua changamoto iliyokuwa inawakabili watoto wetu ya kutembea umbali mrefu kwenda shule ‘’ alisema

Ujenzi  wa shule hiyo unatarajia kukamilika mwezi Disemba mwaka huu ambapo mwakani mwezi wa kwanza itasajiliwa rasmi na kuanza kutoa huduma za kimasomo kwa wanafunzi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI