Header Ads Widget

RICO KUFUNGUA FURSA ZA KIBIASHARA

 



Katika kuhakikisha fursa mbalimbali za kibiashara zinakuzwa nchini kwa lengo la kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kampuni ya Rico Advertising imezindua jarida maalum ambalo linatoa fursa mbalimbali kwa wafanyabiashara......Na fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizindua jarida hilo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Renee Dobbs amesema lengo la jarida hilo ni kukuza biashara mbalimbali za wafanyabiashara ambapo wataweza kuzitangaza bidhaa zao kimataifa.


"Jarida hili litaweza kutangaza biashara za wafanyabiashara mbalimbali kimataifa pamoja na kubadilisha fursa za kibiashara kutoka nchi moja kwenda nyengine, kwani litapatika sehemu mbalimbali muhimu"amesema Renee.


Aidha, amesema kuwa Jarida hilo litatolewa bure na litapatikana kwenye maduka makubwa, balozi mbalimbali zilizopo nchini Tanzania, na nje ya nchi pamoja na hoteli mbalimbali ndani na nje.


"Tutaanza kutoa nakala 3000 ambapo zitapatikana katika sehemu muhimu kama nilivyoeleza hapo juu, tutaanza na ubalozi wa uturuki uliopo nchini Tanzania na baadae tutazifikia balozi zote ili kuhakikisha fursa hizi wafanyabiashara wanazipata Ili kukuza biashara zao"amesema Renee.


Hata hivyo amesema kupitia jarida hilo watakua wanatoa ripoti kwa wafanyabiashara waliojiunga Ili kila mmoja kufahamu maendeleo ya biashara yake, tangu alipoanza kujiunga na jarida hilo hadi ripoti itakapotolewa.


Hata hivyo, amewataka watanzania kujitokeza na kujipatia nakala za Jarida hilo kwa lengo la kujionea biashara mbalimbali zinazopatikana katika jarida hilo, pia ameyataka makampuni mbalimbali kwenda kutangaza bidhaa zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI