BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Nishati na Maji (Consumer Consultative Concil (EWURACCC) limeonya wafanyabiashara wanaowauzia wananchi mitungi ya gesi bila kuwapimia kwenye mizani ....Na Hamida Ramadhan Dodoma
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na katibu mtendaji wa baraza la ushauri la watumiaji wa nishati na maji(EWURA CCC]Mhandisi Goodluck Mmari katika mafunzo kwa watendaji wa kata na mitaa kutoka wilaya ya Dodoma yenye lengo la kujua namna bora ya kutumia huduma.
Mhandisi Mmari amesema asilimia kubwa wanaofanya biashara ya kuuza mitungi ya gesi bila kuwa na mizani ya kupimia ni wale ambao wamevamia hiyo biashara hivyo juhudi za uelimishaji kwa wananchi zimeendelea ili kuhakikisha wananunua mitungi ya gesi inayopimwa.
" Tunashirikiana kwa karibu na Wakala wa Vipimo lengo likiwa ni kuhakikisha wafanyabishara wote wanaojishughulisha na uuzaji wa mitungi ya gesi wanakuwa na mizani ili wasiwaibie wananchi," amesema Mhandisi Mmari
Kwa upande wake afisa msaidizi Uelimishaji na Utawala EWURA CCC Dodoma Amani Mbogo ametoa ushauri kwa wananchi kuacha tabia ya kutumia simu wakati wanapika kwa kutumia mtungi wa gesi kwani yanaweza kutokea madhara ya mlipuko huku.
"Kuongea na simu huku unapika kwenye jiko la gesi kunaweza kusababisha mlipuko katika nyumba yako ulioijenga kwa gharama kubwa hivyo mkiwa kama watendaji nendeni mkatoe elimu hii kwa wananchi wenu kuepuka maafa na gharama kwa ujumla," amesema
Naye Mjumbe wa EWURA CCC Dodoma Monica Mwazembe amesema jumla ya watendaji 62 wa mtaa wamepatiwa mafunzo hayo lengo likiwa ni kwenda kuwafundisha wananchi .





0 Comments