Header Ads Widget

RAIS MWINYI AONGOZA KIKAO CHA KWANZA CHA BARAZA LA MAPINDUZI KATIKA KIPINDI CHA PILI CHA SERIKALI YA AWAMU YA NANE


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 29 Disemba 2025, ameongoza Kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) katika kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Nane.

Kikao hicho kimefanyika Ikulu, Zanzibar, na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Katika kikao hicho, kilichofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Mapinduzi, Rais Dkt. Mwinyi pia ameongoza hafla ya uapisho wa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Mgeni Khatibu Yahya, aliyeteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo.


Kabla ya uteuzi wake, Mhe. Mgeni Khatibu Yahya alikuwa akihudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Pemba.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI