Header Ads Widget

RAIS SAMIA KUHUDHURIA MIAKA 50 YA HOSPITAL YA RUFAA YA BUGANDO MWANZA.

Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku mmoja Mkoani Mwanza. mwandishi wa matukio daima Chausiku Said anaripoti kutokea Mwanza

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel alisema kuwa lengo kuu la kufanya Ziara hiyo ni kuhudhulia Maadhimisho ya miaka 50 ya hospitali ya rufaa ya kanda Bugando.

Ziara ya Rais Samia ni kuhudhuria maadhimisho ya jubilei ya miaka 50 ya hospitali ya rufaa ya kanda Bugando.

Robert alisema kuwa hospitali hiyo ya kanda ina mchango mkubwa kwa watu wa kanda ya ziwa pamoja na  Mikoa ya shinyanga,  tabora, kagera na kigoma kwa kutoa huduma kubwa.

"Hili limepokewa kwa heshima kubwa Rais kuja kuhudhuria katika maadhimisho hayo na inaweka historia kubwa katika utoaji wa huduma za afya" alisema Robert







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI