Header Ads Widget

MADAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YASIO AMBUKIZA WAPIGA KAMBI KWA SIKU TANO MWANZA

Madaktari bingwa wa magonjwa yasio ambukiza wameweka kambi ya siku tano kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wanaojiweza na wasio jiweza. mwandishi wa matukio daima Chausiku Said anaripoti kutokea Mwanza

Bahati Msaki ni Mganga mfawidhi wa hoapitali ya Sekouture ambaye pia ni daktari bigwa wa watoto alieleza kuwa wameamua kuanzisha kambi hiyo maalum kwa lengo la kuwafikishia wananchi huduma kiurahisi na kupata punguzo la bei ya upimaji wa magonjwa mbalimbali.

Alieleza kuwa kutokana na watu wengi  kushindwa kukidhi mahitaji ya upimaji wameamua kuweka kambi na kupunguza gharama ya vipimo ili watu waweze kupima afya zao na kujiweka imara kuliko mtu kushindwa kufahamu anasumbuliwa na ugonjwa gani na kuchukua hatua za haraka.

"Tumeamua kuweka kambi ili kuweza kuwawezesha watu kupima magonjwa yasio ambukizika kwa bei nafuu kabisa ambayo kila mtu anauwezo wa kupima" alisema Bahati.

Bahati alieleza kuwa utoaji wa huduma hiyo wamepanga kuwafikia watu takribani 5000 watakaopata huduma hiyo.

Baadhi ya  wananchi waliofika hospitalini hapo wamepongeza hatua hiyo iliyofanywa na madaktari hao kwani wanatumaini watu wengi watapata matibabu hayo.

Aidha kwa upande mwingine walieleza kuwa hospital hiyo itawasaidia watu wengi kuweza kugundua matatizo yao yanayowakabili.

Pia walitoa wito kwa wananchi kujitokeza kuhakikisha wanapima afya zao na kuhakikisha wanapata matibabu na kuepuka na vifo visivyotarajiwa.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI