Header Ads Widget

OFISI YA ELIMU SEKONDARI MBINGA MJI YAWEKA MIKAKATI YA KUIBUA VIPAJI VYA MICHEZO KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI.


AFISA Elimu wa Sekondari katika Halmashauri ya Mbinga mji Stuart Kuziwa amesema ofisi yake inajipanga  vema kuinua vipaji vya michezo kwa Wanafunzi wa shule za Sekondari za kwenye Halmashauri hiyo na hatimaye kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali yakiwemo ya Umiseta. mwandishi wa matukio daima Amon Mtega anaripoti kutokea Mbinga.

Akizungumza na mtandao wa matukio daima, afisa elimu huyo alisema kuwa ofisi hiyo imefikia kufanya maandalizi ya wachezaji wa michezo mbalimbali kwa kuwaibua wanafunzi kwenye shule zao wanazosoma baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi wanavipaji vya michezo lakini havionekani kutokana na kutokuibuliwa.

Kaziwa alisema kuwa hadi sasa wanafunzi 100 wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu wameshapatikana na siku siyo nyingi watapelekwa kambini ili kuwanoa kikamilifu na mwisho wa siku kuwa na vijana bora wa michezo.

Alifafanua kuwa licha ya kuwa na vijana bora kwenye nyanja za michezo lakini bado katika mashindano ya Umiseta watafanya vizuri kwa kuwa watakuwa wameandaliwa vya kutosha.

Akizungumza kwa mifano afisa elimu huyo alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakiidharau michezo bila kutambua faida zake kuwa ni sehemu ya upataji wa ajira pamoja na kutengeneza afya za wachezaji.

Kwa upande wake mratibu wa mashindano na mtaalamu wa michezo Yovin Mapunda alisema kuwa zaidi ya shule za Sekondari 20 zimehusishwa kikamilifu katika kupata wanafunzi wenye vipaji vya michezo.

Mapunda ambaye pia ni mthibiti ubora wa shule alisema kuwa katika kuwapata wachezaji hao walifanya mabonaza mbalimbali kisha kuwapata wenye vipaji na kuwa wataendelea kuziita timu mbalimbali ikiwemo ya Sekondari Luhuwiko ya Songea kuwachezesha michezo ya kirafiki ili kuwajengea ujasili vijana wao na kuvizoea viwaja mbalimbali vya michezo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI